Kibosho1
JF-Expert Member
- Dec 12, 2017
- 2,621
- 4,293
Kwa kweli tusipompongeza mama kwa utawala wake tutakuwa hatuna shukrani, tumeishi na utawala uliopita tukaona wafanyabiashara na matajiri walikua maadui, wakabinywa wakashindwa kufanya miradi ya maendeleo. Wakashindwa hata kujenga nyumba zao.
Kwa Samia kuna uhuru na njia kibao za kupiga, akili yako ujanja wajo ndio utajiri wako. Ndio maana majumba makali na ya biashara yanajengwa na kuendelezwa kila kona ya nchi. Hiki ndio kipindi cha kufanya mambo ya maana kama ushapiga dili lako. Kuna baa, kuna grosari kila baada ya nyumba 2 na zote zinauza, kwanini tusiseme hela imeingia mtaani? Kuna ofisi kibao za mikopo na watu wanakopa, kuna apps kibao za mikopo yan kiufupi mambo yamekuwa rahisi kuliko mwanzoni.
DP world wanachukua bandari ili kuondoa urasimu uliokuwepo na kuondoa ulegevu wote mambo yaende haraka, natamani sana hata ATCL, TRC NA TTCL yote yabinafsishwe ili yaboreke na yajiendeshe kwa faida.
Kipindi cha mama sio cha kulia tena ni cha kupiga, atakuja rais kama Hayati Magufuli atabana na hali itakuwa ngumu zaidi. Pigeni kazi pigeni dili acheni kulia lia.