RWANDES
JF-Expert Member
- Jun 12, 2019
- 1,788
- 4,401
Kwa sasa siasa za CCM zimeghubikwa na makundi makubwa ambapo kundi la serikali ya awamu ya sita hasa vijana wake wanaoamini CCM ni ya kwao akiwemo NAPE MOSSES NNAUYE wanaweza kuligawa taifa kwa maneno yao kila siku kutoa maneno ya dhihaka kwa kiongozi mkubwa aliyeondoka tarehe 17 March 2021 ikumbukwe kuwa kila binadamu atapita hapa duniani na kila binadamu ataondoka katika njia yake dhana hii ya huyu kijana ambaye inaonesha ndiye amepewa kandarasi ya kumtusi aliyekuwa mkuu wa nchi DR. JOHN POMBE MAGUFULI halina afya kwa chama na serkali kwa ujumla.
Dhana hii si kwamba inawaumiza kundi la ccm tu ambao walikuwa kipenzi chao katka serikali ya awamu ya tano bali wapo viongozi wa juu wa serikali na wananchi kwa ujumla ambao hadi sasa wanahuzuni na kifo hicho kilichotokea mwaka jana.
Viongozi wa serikali huyo kijana wenu awe na akiba ya maneno hakuna aijuaye kesho msemo huu unawaumiza waliokuwa wafuasi wa magufuli hata nyie tafakarini kuhusu msemo huo. Nani anamiliki ya hii nchi mimi nachojuwa hii nchi ni ya watanzania wote sasa demkeni tu kwa maneno ya kejeli yasiyonatija kila mtu anaona kinachoendelea.