Uchaguzi 2020 Kwa sasa Udiwani na Ubunge ni ajira, tutegemee changamoto kubwa kuelekea uchaguzi mkuu hasa ndani ya CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Tunakumbushana tu kwamba kwa sasa hapa nchini siasa ni ajira hivyo wabunge na madiwani tegemeeni changamoto kubwa kutoka kwa toleo jipya.

Ndio hao akina Harmonize, Diamond, Juma Kaseja, Mrisho Mpoto na wengine wengi wanaopiga jalamba muda huu.
Changamoto itaikumba zaidi CCM kwani ndio yenye uhakika wa kushinda kwa 99%

Maendeleo hayana vyama!
 
Mzee Mgaya ccm haina uhakika wa kushinda kwa 90%, sema wanauhakika wa kutangazwa washindi kwa 90%. Kwasababu hawapatikani kwa utaratibu wa kukubalika kwa ridhaa ya wananchi, ndio maana unaona watu wasiosahihi wakiamua kujiiingiza kwenye siasa. Hayo ni madhara ya hizi siasa za kishenzi, na tutakuja kuvuna tunachokihalalisha sasa hivi.
 
Ushindi ni ushindi tu bwashee!
 
Kwa kuwa sifa kuu ya kuwa mbunge hapa Tanzania ni kujua kusoma na kuandika basi demokrasia haina kabisa maana kwani hii inafanya ionekane kuwa karibu kila mtu anaweza tu akawa mbunge.

Na ukiona sampuli za watu ambao Magufuli anawafagilia ubunge ni dhahiri kuwa anatafuta bunge lijalo liwe muhuri zaidi ya hili la sasa, presumably, ili kukidhi malengo yake fulani ya kibinafsi.

Kwa muda mrefu bunge la Tanzania limekuwa na watu ambao hawaelewi nini maana ya kuwa mbunge hasa wale wa chama cha ccm kitu ambacho kimewafanya wawe hawana tofauti na mawakala wa serikali, kama mawaziri pale wanapokuwa bungeni hali ambayo mwakani huenda ikawa mbaya zaidi.
 
Back
Top Bottom