Kwa Sera Mpya ya Elimu, Kuna ulazima wa kuwa na Maafisa Elimu wawili ngazi ya Halmashauri?

Mapambano Yetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
1,130
Reaction score
2,102

Mbona kama kuna mkanganyiko hapa? hii Elimumsingi na Sekondari mbona hazijawa defined vizuri?
 
Nadhani elimu msingi ni ile ya std one mpaka four. Sekondari ni kidato cha tano na sita.

Tusubiri sheria zake
 
Hivi kipi kinaanza kati ya sheria na sera? kwa uelewa wangu inaanza sheria kwanza kisha sera.

Kwa sera hii imetokana na sheria ya elimu namba 10 ya mwaka 1978 na marekebisho yake Na.10 ya mwaka 1995
 
Hivi kipi kinaanza kati ya sheria na sera? kwa uelewa wangu inaanza sheria kwanza kisha sera.

Kwa sera hii imetokana na sheria ya elimu namba 10 ya mwaka 1978 na marekebisho yake Na.10 ya mwaka 1995

Binafsi bado sijawaelewa
 


Mbona kama kuna mkanganyiko hapa? hii Elimumsingi na Sekondari mbona hazijawa defined vizuri?

Ndugu. Neno Msingi lina maana tofauti hapo ilivyotumiwa. Hata hivyo, naona walikosea kiwango fulani, kwani infanya kukanganya. Elimu ya Msingi inamaanisha Basic education.

Kwa hivyo, basic education imetoka Std 7, na ikawa form 4. La pili, Elimu Msingi inamaanisha Primary Education. Wajua neno msingi lina maana mengi. Pia linaweza kumaniisha foundation, au cha kimsingi (the most important.)
 
Sasa kama elimu ya msingi ni std one mpk form 4 kwa miaka kumi kama inavoeleza hapo ipoje, primary education ni ipi na miaka mingapi na secondary ni ipi?

Na kama std 1 mpka four ndio elimu ya msingi ya foundation, iyo ya secondary inaanzia wapi?

Naitafuta sera hii ni isome ila nahs naona madudu sana, nitarud ila nawaza tu vichache ambavyo sijavijua kama:-

mtu akimaliza iyo foundation ambayo ni std 1 mpk form four ya miaka kumi ni lazima aende secondary? Kama aendi akitoka hapo na form four (foundation) yake anaweza kwenda chuo kuanza certificate kama ilivo sasa? Na Kama itakuwa ivo kwa ina maana mtu anatoka elimu ya msingi miaka 10 kisha anaenda elimu ya juu?

Nna mengi sana ya kusema, hadi huko kwenye umri wa miaka minne yaweza kuanza darasa la kwanza ila naitafta nisome kwanza, japo nna vipande vipande mwenye nayo complete tafadhali naomba
 

Mkuu, sera yenyewe ndio hii: https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=227001&d=1424000482

Shule ya msingi itaanza darasa la KWANZA hadi SITA. Baada ya hapo, Kutakuwa na kidato cha KWANZA hadi NNE. Kisha, TANO hadi SITA. Zikiwa pamoja, mtu atakuwa akienda chuo kikuu baada ya kumaliza miaka kumi na miwili. Hii itakuwa sawa na KEnya.

Tofauti ni kuwa, baada ya hapo, Kenya huwa na miaka minne katika chuo Kikuu, na nyinyi mtaendelea kuwa na miaka mitatu. Hii ina maana kuwa, kuna mabo fulani ambayo itabidi myatoe katika silabasi, ili mweze kutupa nje elimu ya mwaka mmoja.

.
 
Binafsi bado sijawaelewa

Kawaida inaanza sera na baadaye kutungiwa sheria (ingawa mara nyingine sheria hutangulia na sera kuundwa baadaye kulingana na mahitaji yatakayojitokeza labda baada mapungufu ya hiyo sheria kuonekana au kuibuka hitaji jipya ambalo halikuonekana hapo mwanzo).

Katikamchakato wa kutunga sera (policy making process) mawazo ya wadau yanatakiwa kukusanywa (public/stakeholders opinion) na hasa wale ambao sera hiyo itawaathiri.

Utungwaji wa sheria hufanywa na Bunge baada ya sera kupitia hatua mbalimbali ikiwemo kushirikisha wadau. Ili sera iwe halali lazima itambuliwe (ihalalishwe) na sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…