Mapambano Yetu
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 1,130
- 2,102
Tamko
3.1.2. Serikali itaweka utaratibu wa elimu ya awali kuwa ya lazima na kutolewa kwa watoto wenye umri kati ya miaka mitatu hadi mitano kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja.
3.1.3. Serikali itaweka utaratibu wa elimumsingi kuwa ya lazima kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne; na kutolewa kwa miaka kumi na umri wa kuanza darasa la kwanza kuwa kati ya miaka minne hadi sita kulingana na maendeleo na uwezo wa mtoto kumudu masomo katika ngazi husika.
3.1.4. Serikali itaweka utaratibu wa kuhakikisha muda wa kukamilisha elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali za elimu baada ya elimumsingi unalenga mwanafunzi kupata ujuzi stahiki kulingana na Mfumo wa Tuzo wa Taifa.
3.1.5. Serikali itahakikisha kuwa elimumsingi katika mfumo wa umma inatolewa bila ada.
5.4. Ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa
Mamlaka za Serikali za Mitaa zitahusika katika uanzishaji, usimamizi na uendeshaji wa shule za elimu ya awali, elimumsingi na sekondari na kutoa taarifa ya utekelezaji kwa Katibu Tawala wa Wilaya husika. Katika ngazi hii kutakuwa na Afisa Elimu anayeshughulikia Shule za Elimu ya Awali na Elimumsingi na Afisa Elimu anayeshughulikia Shule za Sekondari. Aidha, Maafisa Elimu wa Halmashauri watasimamia na kuratibu utekelezaji wa elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi katika maeneo wanayosimamia
Mbona kama kuna mkanganyiko hapa? hii Elimumsingi na Sekondari mbona hazijawa defined vizuri?