Kwa Shilingi milioni 5 mtu anaweza akafanya biashara gani?

Kwa Shilingi milioni 5 mtu anaweza akafanya biashara gani?

kijanamtanashati

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2014
Posts
516
Reaction score
905
Umu kuna wajuzi na wadau wa mambo mbalimbali naona mtaweza saidia katika hili. Shilingi milioni 5 ya kitanzania mtu anaweza akafanya biashara gani ya kumuingizia kipato kizuri. Msada wenu wakuu.
 
Hakuna kiasi cha pesa kitakachokuhakikishia kutoboa biashara kama hujatulia na kujifunza kwanza kwa waliokutangulia hiyo biashara. Mimi nipo Kibaha,nikikushauri wewe uko Dar au Morogoro,mazingira tofauti.

Way forward, ziweke akiba, fanya field mwezi mmoja kwanza
 
Biashara zipo nyingi sana zenye faida.
Mimi kwa 5mil. Sijui muda wako na matumizi yako ya pesa.
Ila tafuta uwakala wa kuuza gesi za oryx, taifa n.k
Au fungu duka la mahitaji ya home sehemu penye kitaa cha watu.
 
]

Wewe unapaswa uchunguze mwenyewe kwanza Kabla ya yote.
Mazingira uliopo biashara gani inafaa ambayo ipo au haipo kwenye mazingira yako?

Eneo gani zuri la biashara utakayo chagua?

Biashara uliochagua mtaji wake unaendana na pesa yako?

Bidhaa utakayo weka itakuwa na wateja?

Biashara iyo inafaida kiasi gani uliochagua?

Chunguza biashara ulizo ona zinafaa mwenyewe kwa kutafuta ushauri kwanza kwa wanaofanya biashara izo Kama Ni kwa marafiki au jirani au ndugu

Alafu rudi mtandaoni orodhesha biashara izo kwa kulidhia mwenyewe ulizo ona zinafaa pia wanajamii forums wakupe ushauri kuhusu namna ya uendeshaji wake faida au hasara au changamoto za biashara iyo ibaki tu wewe kuchagua

Mimi nakushauri chunguza kwanza mwenyewe uko uko kwenu ndio uje mtandaoni maana hatujuwi mazingira uliopo na biashara utakazo elezwa humu mtandaoni utapata wateja au faida au changamoto zitakuwaje
 
Back
Top Bottom