Timu inayopigwa 3-0 nyumbani kwake, timu ambayo haina uwezo wa kubeba kombe lolote nchini mwake, timu isiyo na mfumo wa uchezaji kiwanjani zaidi ya kucheza mpira wa butua butua leo hii ishiriki ligi Moja na timu ambazo ni Mabingwa wa Afrika na pia ni mabingwa wa nchi zao, Je hamuoni taifa linaenda kufedheheshwa kwa aibu kubwa?
Yaani uwaweke Raja Casablanca, Mamelodi Sundowns na Simba kundi Moja unategemea nini hapo? Hawa kina Boco si wanaweza goma kurejea uwanjani kipindi cha pili?
Ushauri wangu hii timu ingejikita zaidi kwenye kombe la Azam Federation angalau inaweza kufika nusu fainal kuliko kwenda kubugizwa magoli na kuliaibisha taifa la Tanzania huko Superleague