Kwa Simba ipo wazi kabisa wachezaji wengi sana wametumika, wamechoka

Metronidazole 400mg

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
941
Reaction score
2,062
Kipindi ZORAN MAKI anakataa karibia timu nzima mlimuona Kama kocha ndezi, mwoga, Hana maono nk .

Kwa uelewa wangu mdogo wa mpira najua timu kubwa na Bora Yoyote duniani msingi wao wa kufikia mafanikio walioeweka (targets ) kama club Ni kuwa na kikosi Bora na yenye ushawishi kuanzia wachezaji, mashabiki na viongozi wote

Kwa timu yangu Hilo hakuna kabisa, kuanzia uongozi, na HASA HASA WACHEZAJI.

Football Ni career fupi Sanaa, nikimaanisha kote duniani, mfano kwa walio tutangulia (ulaya ) mchezaji Bora atacheza angalau 7yrs (at least Kama yupo Bora kweli kweli ) baada ya hapo anapewa mbadala ili maisha yaendelee

Kwa Simba ipo wazi kabisa wachezaji wengi Sanaa wametumika, wamechoka na hata sajili zao bado za mchongo, niwazi wanao sajili hawana taalumu za usajili, kiufundi huwezi sajili washambuliaji TU ambao hata bado hawana efficiency Ni kosa kubwa.

Chama, phiri, kapombe, bocco, saido, miqquisonne na wengine sio wachezaji wa kucheza Simba kabisa, wanajitahidi ila ndio hivyo UMRI UMRI sio rafiki kwao.

Naomba mtu anijibu.....Phiri anacheza namba ngapi kwa ufanisi mkubwa(efficiency)???.....anastahili kuichezea Simba????
 
Miaka 7? Wachezaji wangapi wamecheza kwenye ubora wao kwa zaidi ya miaka 7.
Tatizo letu labda ni umri kuongopa kwa huku kwetu, ila huko majuu mchezaji anaweza kwa tegemeo akiwa na miaka 19-21 na akauwasha mpaka 30+.

Phiri namtetea anacheza popote pale, ni walimu tu, huyo zolan maki mwenyewe hakuwa aakimtumi phiri?

Hoja yako kuwa wachezaji wengi wamechoka naiona ina usahibi kiasi kikubwa, lakini viongozi hawakusajili kwa mikakati, walijisajilia tu, yuko wapi namba 8 mwenye ubora kama wa ngoma!? Hakuna timu nzima halina namba 8 mwenye ubora wa kuendana na wenzie.
 
False number 9.
Kustahili ama kutostahili 50/50

Kwenye suala la umri nakubali pia. japo wapo wenye umri mkubwa na wanakiwasha vizuri mfano namba tatu ya Al ahly Ina umri sijui 36 plus Ile somebody ALLY MAHLUL kama. Japo kwangu naona asilimia ya Hawa "wakongwe" inabidi iwe ndogo na isikaribiane kwa wanaoanza maana Mpira wa sasa unakwenda kwa hesabu , muda , speed wakati wa kufanya transition nk (Mimi sio mtaalamu wajuzi wanayajua) so unawahitaji vijana hasa kwenye beki za pembeni , Midfielders wa juu wanaocheza kama wawinga , na midfielder mkabaji (nyakati mmepokwa Mpira)

Umri lakini una athari zake ...maana inafika mahala akili inataka ila umri hautaki (mwili). uwezo wa kuhimili dakika 100 unacheza umri unakataa au labda ucheze dakika za mwanzo vizuri lakini baadae uanze kutegea.

Na shida Mpira wa sasa unategemea timu nzima kila mmoja atimize jukumu lake pindi akiwa na akiwa hana Mpira. hasa hasa mnapokua mmepokwa Mpira.

Sometimes tunaleta wachezaji kwa tunachoona sisi anacho au YouTube lakini Je mwalimu anapendekeza mchezaji wa aina hiyo ? tunafeli hapo.

Yote kwa yote sidhani Simba tunashindwa kupata defensive midfielder mzuri hapa East and central Africa....kariba ya Mamadou semake nk

Project haijengwi kwa ujanja ujanja huwa inaonekana na kila mtu anaiona. mapenzi/mahaba yakiingilia kati unaharibu kazi.

Simba siku zote 💪💪🦁
 
Wakati uchebe ni kocha wa Simba karibuni wachezaji wote walipewa nafasi ndio maana ya kikosi kipana. Makocha waliofuata wengi walikuwa na kikosi kipana, lakini tunazungumzia uchovu wa wachezaji bila kuzungumzia ujinga wa viongozi kuanzia kufanya usajili Hadi kusimamia timu.
 
Anamaanisha miaka 7 mnaanza kumtafutia mbadala endapo likitokea la kutokea sio kwamba mchezaji anakua tayari aahachoka. Maana kwa mchezaji aliecheza mfululizo kipindi miaka iyo ndo pumzi inaanza kukata kama aliaanza kuwa tegemeo akiwa na miaka 18 basi kwenye 26 mwili utaanza kuchoka mfano michael owen au kama alianza kuwa tegemeo akiwa 23 kwenye 30 hivi mwili utaanza kuchoka mfano kante
 
Naunga mkono hoja, Simba inakosa pasi za uhakika. Timu inacheza pasi nne wananyang'anywa. Umri sawa ila si kwautumbo wa Jana. Inawezekana viongozi hawajatimiza matakwa ya mikataba yao. Hivyo kiujumla project inaanzia kwa viongozi wenye vision. Sasa Musovero na Jaribu Tena, Wana maono gani zaidi ya pension. Mo analiwa pesa zake Bure. Simba kuanzia kwenye timu za vijana hola. Hili tatizo linamisimu miwili Sasa, viongozi ni walewale walioshindwa kulitatua. Kwanini hawaachii ngazi.
 
Nim
Nimekuelewa chief
 
Nitajibu kuhusu Phiri, ni kwamba anahitajika Yanga haraka. Israh Mwenda hakuna kitu, Kapombe ni Bora sana.
 
Timu Bora na inayo jielewa huwezi subiri baada ya miaka 7 ndio umtafutie mchezaji FULANI mbadala......na ndio maana kipindi FULANI robertinho anakuja Simba na kumfanyia SUB chama mashabiki wengi walikereka kwanini??

Ni kutokana na mentality kuwa Chama Ni mchezaji mzuri ila hatukujiuliza huyu Chama atacheza milele???
 
Kwenye mfumo gani mkuu???.....
 
Simba ili iwe Bora......kwanza waondoe wazee kuanzia Sasa Alafu wapewe nafasi vijana......ata Kama watazingua tuendelee kuamini Sanaa Kama tulivyo mwamini kibu deniss

Ikifikia hatua hii ni wazi tutaazisha academy na kuendelea kuamini vipaji ....na mwisho wa siku hatuta sajili wachezaji wa nje Tena......na hata tukisajili Ni mmoja au wawili na awe na uwezo kweli kweli

HII NDIO SIMBA NINAYO IONA MIMI FRANK
 
Simba wanapenda kurudisha wacheza waliowahi kuifunga yanga wakidhani watakuja kuifunga Tena kumbe viwango vyao vimeshuka
 
Kwa vijana simba atabaki Izra Mwenda na Kibu pekee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…