Kwa Simba na Yanga, Mayele ni "mfalme" uwanja wa taifa kwa Mkapa

Kwa Simba na Yanga, Mayele ni "mfalme" uwanja wa taifa kwa Mkapa

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Kinara wa mabao kwenve kikosi cha Yanga na Ligi Kuu Tanzania Bara, Fiston Mayele mwenye mabao 16 hadi sasa, ameifikia rekodi yake ya msimu uliopita na sasa anasaka kuivunja.

Baada ya kukosa tuzo ya ufungaji boramsimu uliopita iliyokwenda kwa George Mpole (Geita) kutamba
na kumaliza msimu aki wa kinara kwa mabao 17, Mayele anaonekana kuwa karibu kuitwaa msimu huu.
Hadi sasa, ikiwa imesalia michezo minne msimu kumalizika, Labda kutokee miujiza pekee itakaomnyima Mayele tuzo ya mfungaji bora kutokana na kasi yake

Habari nzuri kwa Yanga na mbaya kwa Simba ni kwamba katika magoli 16 aliyoyafunga Mayele, 11 ameyafunga katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, na katika magoli yote hakuna goli la Penati hata moja.

Katika mabao 11 aliyofunga mshambuliaji huyo kwenye Uwanja wa Mkapa, mabao 6 ameyafunga kipindi cha kwanza na 5 kipindi cha pili.

Tuko hapa tunasubiri kuona kama ataendeleza moto wake

yangasc_279391222_365715012269430_4336586080698701116_n.jpeg
 
Back
Top Bottom