Kiti cheupe
Member
- Apr 8, 2024
- 5
- 5
Nimeona video clip ambayo muheshimiwa waziri Kabudi anazungumza nia ya wizara yake kusimamia mchakato wa kuufanya mziki wa SINGELI kuwa mziki rasmi wa kuitambulisha Tanzania jambo ambalo sio sahihi kwa sababu zifuatazo:
Kwanza kabisa tayari Tanzania ina mziki unaoitwa Bongo fleva unaoitambulisha kwa miaka mingi na umeleta tuzo nyingi hapa nyumbani kupitia wasanii mbalimbali kama Ali Kiba, Diamondi, Ray van, Harmonize, Lady jaydee. Nk.
Huko duniani tayari watu wanajua mziki wa Tanzania ni bongo fleva.Nchi kubwa kimziki kama Nigeria., Afrika kusini na Ghana wanajua watanzania wanaimba bongo fleva.
Hivyo tusiwachanganye watu kwa kuwaletea jina jipya la mziki wakati tayari tumeshatengeneza Brand ya Bongo fleva.
Sababu ya pili ni ishu ya MAADILI. Japo Bongo fleva pia ina upungufu wa maadili kwa baadhi ya wasanii LAKINI mziki wa SINGELI una maporomoko ya kimaadili.
Huwezi kukaa sebleni na wageni ukaangalia mziki wa singeli yaani kuna vitendo vya kingono kuanzia mwanzo mpaka mwisho.
Mbaya zaidi mashoga wengi wanatokea kwenye mziki wa singeli kuliko bongo fleva. Ni ngumu kukuta mziki wa bongo fleva kuna mashoga wanakata mauno ni singeli tu labda na taarabu.
Sababu ya tatu ni ujumbe.
Nyimbo nyingi za singeli hazieleweki zinaimba nini, kwa kifupi hazina ujumbe. Licha ya kuimba sana mapenzi lakini wasanii kama Diamond, Ali Kiba na Harmonize wameimba nyimbo nyingi zenye ujumbe.
Sasa tafuta singeli 10 ambazo zimewai kuimba ujumbe wa kuelimisha jamii kwa ufupi utaanza kuhesabu vidole hadi zifike 10.
Sababu ya mwisho ni uelewa.
Wasanii wengi wa bongofleva wanajitambua na wamesoma angalau sekondari na baadhi hadi vyuo vikuu kama wakina MwanaFA, Roma, Nikki 2, prof jay, Lakini wasanii wa singeli wengi wao walikataa shule na wametokea kwenye mazingira yaliyozungukwa na uhalifu kama uvutaji bangi, madawa, ukahaba n. K
Nihitimishe kwa kusema muheshimiwa waziri haujui huu mziki hivyo anadhani ni mziki tu kama ilivyo mingine. Mlionae karibu mumshauri tafadhali kabla hajaaribu.
Kama kuna mtu anang'ang'ania Singeli atuambia ni tuzo ngapi za kimataifa zimepatikana kupitia Singeli?