Aisee watanzania sisi tuna matatizo, nadhani ndo maana tuna sua sua kwenye biashara. Baada ya kuangaika sana na mshikaji kutoka US kutafuta gari mitandaoni (shida haswa ni kuwa gari hazina details za kutosha yaani mpaka mpigiane simu sana) nikaamua kutumia elimu yangu kutengeneza website ya kutangaza magari bure. Yaani muuza magari aumizi kichwa, details zote anaweza weka kwa kuweka tick sehemu husika. No hustle.
Tena nikaweka sehemu mbili za ku register yaani kwa muuza gari lake binafsi, na kwa wafanya biashara za kuuza magari (dealers)
Lakini bwana,
duu watanzania wavivu, unamweleza mtu anaipenda frsh kabisa ila anataka wewe ndo mpigie picha magari yake na kumwekea mtandaoni. Sasa unajiuliza yaani nikutengeneze website kwa ajili ya wewe kufanya biashara bure kabisa, bado tena nikuweke magari? Really??
Mwingine anakwambia biashara ngumu. haa, yaani haelewi kuwa hiyo ni sababu tosha kutumia hiyo website (www.bongocars.com)
Yaani ni shida. Nikaongeza features kama za kuwasilianza na muuza mgari humo humo kwenye website (messaging) na hata kwa email pia bado ni shida. Picha unaweza weka mpaka ishirini kwa gari moja bado shida.
Alafu nilitaka kuweka sehemu ya kuomba mkopo wa gari, kupata bima ya gari na pia huduma ya kusafiri gari east africa ila kusema kweli nimevunjika moyo.
Kuna maelezo ya kwanini hii website ni nzuri hapa
Bongo Cars - 10 Reasons you should use Bongocars.com
Sasa nataka kutengeneza ya
hoteli, guest house, lodge, hostel na hata watu wa tour ili waweze pokea booking na hata malipo online, hii nikutokana na shida ninayoipata (ambayo na nadhani wengi tunapata shida hiyo) ya kusafiri bila kujua utafikia wapi. Hasa pale unapofika usiku.
Ingawa hata ukifika mchana unajikuta umelala sehemu ya bei ya juu au huduma mbaya kwa sababu hujui sehemu nyingine. Ila sina imani na watanzania
Nimejaribu kuandika maelezo yake hapa
Neema kwa wenye Hoteli, Guest house, lodge, hostel, apartments na utalii
kuona kama itapata watu hasa wanojishughulisha na biashara hiyo (nimeweka form ya kujaza) ili nisijitese bure kama ya www.bongocars.com
NB: Naona comments nyingi zina suggest matangazo, naona tufanye hv, ingia kwenye website (www.bongocars.com) utaona icons za kushare, click share kwenye groups za whatsapp, facebook na kadhalika, then nitakuja kuleta mrejesho.