Kwa style hii tusahau mpira wetu kupiga hatua

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Posts
24,314
Reaction score
38,919
Anaandika Khaled Msabaha#ThePointGuard

FB_IMG_1544872821316.jpg
Vitu vingine huwezi kuviona nchi nyingine bali utaviona Tanzania tu, kweli mtoto usiempenda ndio anayekuja kukuletea mafanikio na utaona aibu kwa yale uliyomfanyia.

Wakati kikosi cha Serengeti Boys kikiondoka Tanzania kuja Botswana TFF hawakutangaza habari yoyote kuhusu safari hii wala kuitisha press conference kuongelea safari ya Serengeti Boys, hii ni timu ya taifa mgeiaga kama timu nyingine basi mngewatangazia watanzania habari kwamba timu inasafiri.

Lakini licha ya yote timu imesafiri bila mkuu wa msafara matokeo yake timu imefika Botswana hata ada ya mashindano TFF hawajalipa na hakukuwa na jinsi waandaaji wakakataa kutoa Malazi kwa wachezaji na hivyo timu nzima ikalala ndani ya basi wachezaji wakaamka asubuhi miguu imevimba alafu kesho yake ndio mechi ya kwanza na Angola.

Tunashukuru ada ililipwa siku moja kabla ya mechi hivyo kukawa na uhakika wa kushiriki mashindano lakini mlisababisha wachezaji washindwe kuwakabili Angola na kufungwa goli 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wa kundi B.

Yote haya yasingetokea kama timu ingesafiri na mkuu wa msafara kwani angehakikisha anashughulikia taratibu zote lkn matokeo yake kocha Oscar Mirambo akapambana kwa kila kitu mpaka mambo yakaenda sawa, kwa ujinga wangu nilidhani TFF wangemsafirisha mtu mapema akashughulikia kila kitu mapema na timu ingefika kwa kazi ya kucheza tu yasingetokea yote yale.

Lkn watoto hawa wanaojua thamani ya bendera ya taifa lao walipambana na kuhakikisha hawafungwi tena wakamfunga Malawi 2-1 kisha Sauth Afrika 2-0 na kufuzu nusu fainali, napo wamemtoa Zambia kwa penati 5-4 baada ya sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Hapo ndio utajuwa kwann nakwambia vitu vingine utaviona Tanzania tu,

TFF sasa ndio wanaposti kwenye social media eti Hongereni Serengeti Boys kwa kutinga fainali. Ninamashaka na hongera hii.

Kiukweli TFF mmefeli mlipaswa kuwatangazia watanzania tangu safari lkn cha ajabu hata waandishi wa habari hawakuwa na taarifa kwamba Serengeti Boys imesafiri kwenda Botswana kwenye michuano ya Region 5 Youth Games 2018 Gaborone. Mliwatelekeza lkn vijana hawajali wanapambana.

Hongera Morice Abrahamu hongera Kelvin John kwa kutwaa tuzo ya mchezaji ndani ya mechi 3 mfululizo.
 
Aibu kubwa sana,TFF wanahangaika tu na mambo ya Simba na Yanga na Taifa stars menngine hawana hata habari
 
Anaandika Khaled Msabaha#ThePointGuard

View attachment 968912Vitu vingine huwezi kuviona nchi nyingine bali utaviona Tanzania tu, kweli mtoto usiempenda ndio anayekuja kukuletea mafanikio na utaona aibu kwa yale uliyomfanyia.

Wakati kikosi cha Serengeti Boys kikiondoka Tanzania kuja Botswana TFF hawakutangaza habari yoyote kuhusu safari hii wala kuitisha press conference kuongelea safari ya Serengeti Boys, hii ni timu ya taifa mgeiaga kama timu nyingine basi mngewatangazia watanzania habari kwamba timu inasafiri.

Lakini licha ya yote timu imesafiri bila mkuu wa msafara matokeo yake timu imefika Botswana hata ada ya mashindano TFF hawajalipa na hakukuwa na jinsi waandaaji wakakataa kutoa Malazi kwa wachezaji na hivyo timu nzima ikalala ndani ya basi wachezaji wakaamka asubuhi miguu imevimba alafu kesho yake ndio mechi ya kwanza na Angola.

Tunashukuru ada ililipwa siku moja kabla ya mechi hivyo kukawa na uhakika wa kushiriki mashindano lakini mlisababisha wachezaji washindwe kuwakabili Angola na kufungwa goli 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wa kundi B.

Yote haya yasingetokea kama timu ingesafiri na mkuu wa msafara kwani angehakikisha anashughulikia taratibu zote lkn matokeo yake kocha Oscar Mirambo akapambana kwa kila kitu mpaka mambo yakaenda sawa, kwa ujinga wangu nilidhani TFF wangemsafirisha mtu mapema akashughulikia kila kitu mapema na timu ingefika kwa kazi ya kucheza tu yasingetokea yote yale.

Lkn watoto hawa wanaojua thamani ya bendera ya taifa lao walipambana na kuhakikisha hawafungwi tena wakamfunga Malawi 2-1 kisha Sauth Afrika 2-0 na kufuzu nusu fainali, napo wamemtoa Zambia kwa penati 5-4 baada ya sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Hapo ndio utajuwa kwann nakwambia vitu vingine utaviona Tanzania tu,

TFF sasa ndio wanaposti kwenye social media eti Hongereni Serengeti Boys kwa kutinga fainali. Ninamashaka na hongera hii.

Kiukweli TFF mmefeli mlipaswa kuwatangazia watanzania tangu safari lkn cha ajabu hata waandishi wa habari hawakuwa na taarifa kwamba Serengeti Boys imesafiri kwenda Botswana kwenye michuano ya Region 5 Youth Games 2018 Gaborone. Mliwatelekeza lkn vijana hawajali wanapambana.

Hongera Morice Abrahamu hongera Kelvin John kwa kutwaa tuzo ya mchezaji ndani ya mechi 3 mfululizo.

Muda siyo mrefu utasikia wanasiasa nao wanajitokeza ili kujihusisha na mafanikio haya...utasikia kamati imeunda yenye matajiri, watangazaji na baadhi ya watu 'maarufu' ili eti kuweka mikakati ya ushindi...ovyo kabisa....Watanzania watu wa ajabu sana na hasa hawa walioko kwenye nafasi nyeti za maamuzi...nyie subiri mtasikia kamati ya ushindi inaundwa na waziri...
 
Back
Top Bottom