KWELI Kwa taarifa yako… uking’atwa na nyoka huruhusiwi kufunga kamba juu ya kidonda

KWELI Kwa taarifa yako… uking’atwa na nyoka huruhusiwi kufunga kamba juu ya kidonda

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Kumekuwepo na chapisho ambalo limechapishwa na chombo cha habari cha Azam tv tanzania kikiwa nukuu ya kuwa uking’atwa na nyoka huruhusiwi kufunga kamba juu ya kidonda, kuchanja wala kunyonya sumu kwa mdomo. Unachopaswa kufanya ni kutulia kwanza ili kupunguza msukumo wa damu.
Dai hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Elimu na Uhamasishaji Uhifadhi wa Nyoka Tanzania (TASCEA), Aldo Charles, wakati akifanya mahojiano na kipindi cha Morning trumpet
Je ni upi uhalisia wa dai hilo?

Screenshot (1).png
 
Tunachokijua
Kuumwa na nyoka kunaweza kuwa hatari na wakati mwingine kuhatarisha maisha, hivyo kunahitaji matibabu ya haraka na sahihi. Hata hivyo, waathirika wengi hupona kabisa bila kuhitaji dawa ya kupunguza sumu (antivenom).

Nyoka hatari kwa binadamu

Inaelezwa kuwa Nyoka wengi si hatari kwa binadamu. Ni takribani 15% tu ya nyoka duniani na asilimia 20 nchini Marekani wanaoweza kung'ata na kuacha sumu kwenye mwili wa binadamu, hawa huitwa nyoka wenye sumu (venomous).

Idadi ya watu wanaofariki kutokana na madhara ya kung'atwa kwa nyoka

Shirika la Afya Duniani linaeleza kuwa waathirika wengi hawafiki vituo vya afya au hospitali na badala yake hutegemea matibabu ya jadi. Hata hivyo, takwimu zinaonyesha kuwa watu milioni 4.5 hadi 5.4 huumwa na nyoka kila mwaka. Kati yao, milioni 1.8 hadi 2.7 hupata madhara ya kiafya, na watu kati ya 81,000 hadi 138,000 hufariki kutokana na madhara hayo.

Mtu anapaswa kufanya nini anapong'atwa na Nyoka?

Tovuti ya kliniki ya Mayo inaeleza kuwa mtu anapokutana na kadhia hiyo anapaswa kufanya yafuatayo;
  • Ondoka (nenda) mbali na nyoka haraka iwezekanavyo.
  • Tulia na epuka kusogea sana.
  • Vua vito, saa au nguo zinazobana kabla uvimbe haujaanza.
  • Kaa au lala ili sehemu iliyoumwa iwe katika hali ya kawaida na ya utulivu.
  • Safisha jeraha kwa sabuni na maji, kisha lifunike kwa bandeji safi na kavu bila kubana sana.
Je, ni kweli mtu aliyeumwa na nyoka hapaswi kufunga kamba ama kuinyonya sumu hiyo?

Taasisi ya African snakebite inaeleza kuwa hupaswi kulikata jeraha au kuinyonyonya sumu kwa sababu Sumu ya nyoka hushikamana haraka sana na tishu za eneo lililoumwa na kufyonzwa kwenye mfumo wa lymphatic, hivyo utakaponyonya ni kiasi kidogo sana kinaweza kuondolewa kwa kunyonya. Kukata jeraha kunaweza kuongeza hatari ya maambukizi ya ziada.

Inaelezwa pia haishauriwi kufunga jeraha kwa kamba ili kubana damu kwani sumu ya nyoka haisafiri kwa kupitia mishipa ya damu bali zaidi husambaa kupitia tishu hivyo hakuna ushahidi kwamba kufunga kamba kama inaweza kuuokoa maisha.
hili swala la kukaa nakulala ili sehemu iliyoumwa iwe katika hali ya kawaida na kustarehesha liangaliwe upya kustarehe kupi huko wanakusema ikiwa umeng'atwa na nyoka.. hapo ni kijasho chakutoka hovyo, mapigo ya moyo mputa mputa kama gari aina ya tata.. kuna vitu vyakustarehe nyie muda mwengine muwe mnaandika vitu kutokana na uhalisia, huyo alieandika sidhani hata kama alishawahi kuumwa na nyuki ndio uje ustarehe kwa nyoka labda nyoka wa kibisa..😅
 
Juzi nili pigwa jino na nyoka, mkononi gafula nakuta mkono unakufa ganzi kuangalia vizur

nakuta alama ya meno mawili sijakaa sawa naangalia pemben nyoka yule anaishia zake
nikavuta kamba ya bukta nikafungu nikawai petroli nikapaka asee maumivu yake balaa gafla mkono mweus tii ila haikuchukua muda nikawa sawa, nikamsaka mpaka nikampata nikamkata mkia nikaishia zangu sipendag utoto kwenye mwili wangu
 
Sababu zilizotajwa hazina mashiko na hata huyo aliyefanya huo utafiti hajawahi kung'atwa na nyoka. Nge tu akikuweka hukai sawa
 
Kumekuwepo na chapisho ambalo limechapishwa na chombo cha habari cha Azam tv tanzania kikiwa nukuu ya kuwa uking’atwa na nyoka huruhusiwi kufunga kamba juu ya kidonda, kuchanja wala kunyonya sumu kwa mdomo. Unachopaswa kufanya ni kutulia kwanza ili kupunguza msukumo wa damu.
Dai hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Elimu na Uhamasishaji Uhifadhi wa Nyoka Tanzania (TASCEA), Aldo Charles, wakati akifanya mahojiano na kipindi cha Morning trumpet
Je ni upi uhalisia wa dai hilo?

View attachment 3570459
Hii ni kitu kipya kwangu. Kwenye jamii zetu tumeaminishwa sana umuhimu wa kufunga na kamba eneo baada ya jeraha, ili kuzuia sumu isisafirishwe mwilini. Kumbe sio sahihi. Ni vizuri hii Elimu mpya iwafikie wengi.
 
Hawawezi fanya hivyo kwa Sababu hata wao wanaona Haina uhalisia. Kwa mfano ukiwa pori na umenga'atwa UnawezAje lala ili kustarehesha jeraha? Ukisubiri kifo?
 
Hawawezi fanya hivyo kwa Sababu hata wao wanaona Haina uhalisia. Kwa mfano ukiwa pori na umenga'atwa UnawezAje lala ili kustarehesha jeraha? Ukisubiri kifo?
Sasa tunafanyaje?

Mimi na wengine tuliaminishwa kuwa huduma ya kwanza kwa aliyeng'atwa na nyoka ni kumfunga na kamba au chochote kile ili kuzuia sumu isisambae mwilini. Sayansi mpya inasema sio sahihi kufanya hivyo. Sasa hii ndio nashauri iwafikie wengi.
 
Dawa ya mtu aliyeng'atwa na nyoka ni hii tafuta mti wa mbudika uliojikaukia wenyewe polini chukua vipande vichache, chukua na mungu ga nzoka changanya na mbundika na mungu ga nzoka kaanga mpaka yawe majivu yote, tafuta nyoka anayeitwa kipili aliyeuliwa usiku, mbanike,chukua kipande kidogo changanya na mchanganyiko wa mbudika na mungu ga nzoka twanga na ongeza mafuta ya kondoo kidogo, twanga twanga twanga hadi mchanganyiko uwe mmoja. Weka kwenye chombo cha kuhfadhi dawa. Chukua dawa kidogo changanya tena na mafuta ya kondoo kdg kata mahala alipong'awa wasukuma tunaita salago, paka dawa na nyingine mnyweshe. UTAKUJA UNISHUKURU. Seran sambaza huu ujumbe kwa wasukuma wengine
 
Sasa hiyo mimea tutaijuaje sisi tusiofahamu kisukuma?
Na wakati unatafuta hiyo miti na kutafuta mafuta ya kondoo na nyoka kipili, bado aliyeng'atwa na nyoka anaendelea tu kusubiria?🤷‍♂️🤷‍♂️🤷‍♂️
 
Huu utafit nna waswas nao. haiwezekan ustareh wakat israel yupo langon
 
Nakataa usije jidanganya kulala wakati umetoka kung'atwa na nyoka, huo ndio utakuwa mwisho wa maisha yako.
 
Sasa hiyo mimea tutaijuaje sisi tusiofahamu kisukuma?
Na wakati unatafuta hiyo miti na kutafuta mafuta ya kondoo na nyoka kipili, bado aliyeng'atwa na nyoka anaendelea tu kusubiria?
tayarisha dawa yako sasa, kesho/kesho kutwa anaweza kung'atwa jirani yako,ndugu yako au wewe mwenyewe
 
Back
Top Bottom