Kwa tabia hizi chafu za Viongozi na Mashabiki wa Yanga, TFF wakizinduka tutaadhibiwa

Kwa tabia hizi chafu za Viongozi na Mashabiki wa Yanga, TFF wakizinduka tutaadhibiwa

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
2,254
Reaction score
5,161
"Kwa sasa TFF tushukuru wamelala au wana woga. Kitendo tulichofanya juzi uwanja wa Sokoine hakikuwa sahihi. Ifikie hatua tuwe wakweli. Ifikie hatua tuangalie mpira na mchezo wa Mpira na si Ushabiki.

Goal tulilopata kiukweli halikugusa mstari lakini refa kama binadamu alitupatia goal hilo na tukashukuru. Mbeya City penalty yao haikuwana utata why tuchochee fujo? Kwa nini hizi team kubwa zinaamini zenyewe tu zinatakiwa kushinda?

Mi nakumbuka penalty tuliyopata dhidi ya Simba mwaka jana haikuwa halali. Simba mbona hawakufanya fujo? Faulo ilifanyika nje ya box refa akaingiza ndani iwe penalty.

Simba walitulia na Onyango akaja kusawazisha dakika za jioni kwa kichwa. Simba hawakufanya fujo. Kwa nini sisi huwa tunapenda kulazimisha kila kitu?

Na makocha wameshajua saikolojia ya wanayanga. Huwa wanajifichia humo. Nao wnakimbilia kulaumu marefa ili kuficha udhaifu wa mbinu zao. Juzi ukiangalia ile match kocha aliingia na mbinu gani?

Tukumbushane kombinesheni ya Kisinda na Fiston ilikuwa ime-fail. Sarpong alikuwa anafanya mambo ya hovyo tu uwanjani. Hivi ni matches ngapi tumebebwa katika ligi mpaka kufika hapa tulipo?

Ifikie hatua tuelezane ukweli. Kama TFF inaogopa basi tusijizoeze hivi matches za kimataifa tutaumia sana. Maana hii tabia sasa ni kama inaota mizizi. Mashabiki, wachezaji na viongozi wanalazimisha ushindi au wanaamini ni lazima washinde.

Inapotokea kinyume watu wanapanic. Na malalamiko ya kipuuzi huku ukweli ni kuwa team yetu ni mbovu. Tuelezane ukweli tu.

Kama ntaonekana mimi si Yanga kwa kuandika hivi acha iwe hivyo. Niiten majina yote ila ukweli ndo humu. Na kwenye group mkitaka kunitoa mnitoe tu. Ila ukweli ntausema."
 
Hivi hizi threads zote (threads after threads) ni kwa sababu Yanga SC kadroo[emoji28][emoji28]
 
Aliyelalamika ni nani? Hao mashabiki wachache walio jitokeza hapo uwanjani ndiyo ionekane mashabiki wote wa Yanga tunalalimika na kufanya fujo?

Ni kweli Yanga haikucheza vizuri kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya ubovu wa uwanja, na pia baadhi ya wachezaji kama huyo Sarpong na Fiston kupuyanga tu uwanjani, muda wote wa mchezo.

Kuhusu goli na penati, vyote vilikuwa ni halali. Ule mpira uliokolewa ndani. Na kuhusu penati, ilikuwa ni penati halali baada ya Yassin Mustafa kukosa umakini eneo la hatari.

Mimi nakushauri tu waache wachezaji na benchi la ufundi wafanyie kazi changamoto zilizo jitokeza. Mpira wa miguu una matokeo 3! Tumepata sare ugenini, bado tunaongoza ligi, timu inajipanga kwa mechi ijayo.
 
Yule kocha wenu wala hakukosea.

Hamna tofauti na nyani..
 
Yes, hiyo Ni wake up call, kiufupi ni kuwa lazima tuangalie mzizi wa hayo yote upo TFF namna inavyoikandamiza baadhi ya timu na kuhalalisga baadhi ya timu. Nakumbuka TFF hii hii iliunda sheria ya kumbana Mwingi Zahera asivae pensi benchini lakini mpaka Leo tunaona wapo makocha Wana vaa wanavyotaka.

Hii TFF ilisema kuwa Kuna sheria ya mtu akipata kadi nyekundu achague mechi atakazokosa, hii ni baada ya ajib wa Simba kula Umeme, Ili acheze kwenye Simba na Yanga. Na baada ya hapo sheria hiyo ikafa.

Hii TFF bado haijatoa adhabu kwa Mkude wa Simba na Morrison wa Yanga ambayo waliipeleka kamati ya maadili lakini kesi hii mpaka Leo
Hii TFF haijatoa maamuzi malalamiko zaidi ya 5 yaliyoletwa na Yanga 2018

Hii TFF haijailipa Lipuli Pesa ya mshindi wa pili Azam federation tangu 2018,sijui Kama Namungo yeye kapewa au naye kakopwa Kama Lipuli.

Kwa kweli hii TFF imewekwa mfukoni na baadhi ya watu. Imagine mwenyekiti wa Bodi ya ligi mzee kisongo anasema "tuliisahau Yanga kuipaNga kwenye ratiba"kama Yanga inasahaulika je vipi Gwambina na timu za Daraja la kwanza?

Ukihoji Sana mwenyekiti wa TFF anasema tuna "utundulissu" come-on guys! TFF[emoji706]
 
Umeogea ukweli mtupu mkuu! Yanga wana shida aisee! Timu kubwa kama Yanga walishindwa kupata goli 2 au 3 mbele ya vibonde wa ligi ndani ya dakika za mchezo alafu mnakuja kumlalamikia refa ilihali hata goli leyewe walipewa tena dakika za jioni!? Hii i aibu kubwa!
Alafu nimshauri kocha wa Yanga naona nae anataka kupita njia alikopita Mwinyi Zahera.

Kocha lazima atambue kuwa ubingwa wa ligi haupatikani kwa kutamka kwa maneno kwamba sisi mabingwa! La hasha! a wala ubingwa haupatikani kwa ushindi wa mechi moja au mbili, bali ubingwa unapatikana kwa agregate ya ushindi wa asilimia kubwa ya mechi zote za ligi, sasa hii ya kuanza kujitangaza kuwa Yanga jni mabingwa wakati bado una mechi lukuki tena unashinda kwa mbinde inatoka wapi??
 
Kwenye group moja niliandika mtizamo wangu juu ya baadhi ya wachezaji wa Yanga yetu hii niliishia kuonekana mamluki, kuna admn moja mjinga sana anataka tuwe tuna sifia tu wakati kuna wachezaji wanalipwa hela ndefu hawana msaada wowote kwa team. Waliishia kunitoa kwa group nikasema afadhali bakini na ujinga wenu humo.
 
Kuna mechi mbili za Yanga zitakazo fuata zitaamsha Bundi pale Jangwani"Mungu ajaalie iwe kweli"aamin"
 
Wewe ni shabiki wa Mbumbumbu FC. Siyo shabiki wa Vyura FC wewe!
 
Soka la Tanzania limejaa mataahira, kuanzia viongozi hadi mashabiki. Nilishangaa sana eti unagomea nembo ya mdhamini kwa kuwa haina rangi unazozipenda. Huu ni utaahira mwingine.

Kila kiongozi, kocha, refa na wachezaji Wana timu, eidha Simba au Yanga, halafu hujuma huanzia ndani ya moyo wa mtu
Umeongea jambo sensitive na mtu asiye na akili ukiongea jambo la akili kama wewe ni Simba atasema siyo Simba ni Yanga. Kama ni Yanga watakwambia wewe si Yanga ni Mnyama. Maana yake hawataki watu wenye akili.

Ni mpira wa kizamani unagomea nembo sababu ya Rangi. Ni akili za kipumbavu. Yanga ipo na itaendelea kuwepo.

Tubadilike. Wale viongozi wenye njaa wanaotaka tumia hizi team tuwakatae. Hawatusaidii. Wanafanya siasa kwenye mpira. Mpira hautaki siasa.
 
Soka la Tanzania limejaa mataahira, kuanzia viongozi hadi mashabiki. Nilishangaa sana eti unagomea nembo ya mdhamini kwa kuwa haina rangi unazozipenda. Huu ni utaahira mwingine.

Kila kiongozi, kocha, refa na wachezaji Wana timu, eidha Simba au Yanga, halafu hujuma huanzia ndani ya moyo wa mtu
Sihitaji ushahidi mwingine zaidi ya huu kwamba Yanga imejaa mabogas
 
Back
Top Bottom