Kwa Takwimu hizi, CHADEMA bado ni Chama kichanga sana

Mkuu taratibu, tunaomba utujibu haya maswali, kama kweli chama tawala kina wanachama wengi kama unavyojinasibu,

Ni kwanini:

1. Walitumia mbinu ya kuwaengua asilimia 90% ya wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita??

2. Walitumia nguvu ya jeshi la polisi kufanya yaliyofanyika kwenye vituo vya kupiga kura??

3. Walizuia asilimia 80% ya mawakala wa wagombea wa upinzani kufanya kazi yao kikamilifu??

4. Walijaza kura feki kwenye masanduku ya wapiga kura kabla ya kuanza upigaji kura kuanza??

5. Waliandikisha watoto na marehemu kwenye daftari la wapiga kura??

6. Walitumia wizara ya Tamisemi kusimamia uchaguzi badala ya tume huru ya uchaguzi??

7. Walitumia mawaziri, viongozi wakuu wastaafu, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kufanya kampeni??

Tafadhali tunasubiri majibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…