Mizania
JF-Expert Member
- May 17, 2023
- 3,812
- 3,277
Mkuu taratibu, tunaomba utujibu haya maswali, kama kweli chama tawala kina wanachama wengi kama unavyojinasibu,Je, wajua kwamba Chadema kwenye kanzi data yao ina wanachama wasiozidi 450,000 nchi nzima.
Hivyo, ukitazama ndani ya miaka 32 ya kufanya siasa nchini CHADEMA inasajili wanachama 14,062 tu kwa mwaka.
Kama utagawanya tena hiyo 14,062 kwa mikoa 26 CHADEMA ina wastani wa wanachama 540 kwa kila mkoa hivyo ukitazama mkoa kama wa Dar es Salaam yenye wakaazi zaidi ya milioni 6, utagundua CHADEMA ina wanachama wachache sana kwa ngazi ya mkona, chini ya asilimia 3
Hapo sijaamua kushuka kwenye ngazi ya wilaya, kata, vitongoji, mitaa na vijiji.
Ni wazi kwaamba CHADEMA bado ni chama kichanga sana licha ya kufanya siasa kwa muda mrefu kidogo lakini ajabu ni kwamba kijitutumua kuonesha ukubwa ambao kimsingi hakina.
Ushauri wangu kwao warudi kwenye drawing board upya kuangalia wanakosea wapi na namna gani wanaweza kurudi tena kwenye kufanya siasa za ushindani.
Na wajue kwamba, kwa makubwa aliyoyafanya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kati ya 2021 - 2024, CCM itashinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu 2025 na hii ni kutokana na matokeo mazuri ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 2024.
USSR
Ni kwanini:
1. Walitumia mbinu ya kuwaengua asilimia 90% ya wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita??
2. Walitumia nguvu ya jeshi la polisi kufanya yaliyofanyika kwenye vituo vya kupiga kura??
3. Walizuia asilimia 80% ya mawakala wa wagombea wa upinzani kufanya kazi yao kikamilifu??
4. Walijaza kura feki kwenye masanduku ya wapiga kura kabla ya kuanza upigaji kura kuanza??
5. Waliandikisha watoto na marehemu kwenye daftari la wapiga kura??
6. Walitumia wizara ya Tamisemi kusimamia uchaguzi badala ya tume huru ya uchaguzi??
7. Walitumia mawaziri, viongozi wakuu wastaafu, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kufanya kampeni??
Tafadhali tunasubiri majibu.