comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 9,019
- 6,825
Harakati za CHADEMA kwenda ikulu na kupata nafasi ya kutawala nchi hii hazitakaa zifanikiwe sababu walianza na mguu mbaya.
KWANZA - Kuweka misingi yao kwa kubadirisha wanaharakati na uanaharakati kuwa wanasiasa na siasa. huu mchakato huchukua mda mrefu kufaniakiwa.
PILI - Kushobokea siasa za ukanda huku wakisahau kutambua kwamba kanda zao pendwa zina idadi ndogo sana ya watu.
TATU - Kuegemea wasomi, idadi ya wasomi nchi hii ni ndogo sana, wanadharau na walishakata mahusiano na watu wa kawaida wala hawaaminiki kwao. hapa wanapigwa na nguvu ya wajinga- the power of the stupid.
NNE - Kuegemea watu wa mijini, kosa lilelile- watu wa mjini ni 25-30 % ya idadi ya watanzania wote; hawa hawatoshi kukupeleka ikulu hivyo kuwaacha CHADEMA na sifa za kijinga za kufutia machozi za MAJIJI NA MIJI MIKUBWA YOTE IKO CHINI YA CHADEMA.
TANO - Kuwategemea vijana, dunia nzima takwimu zinaonyesha kuwa vijana hawana mda na siasa kwa sababu hazijibu maswali ya maswahibu yao.
SITA - Kuwategemea wapiga dili- hili nimeliona kwa Lissu na hadithi yake ya sembe, mchele, na mchicha vimepanda bei. Vilikuwa chini kwa sababu wakulima wanaovilima walikuwa wakipunjwa bei kwa kuwepo kwa soko finyu.
Sasa soko limepanuka, bei kwa makulima imepanda na kwa mlaji imepanda pia. Kwa kuunga mkono bei ya sembe ishuke ni sawa na kusema mkulima arudi kwenye bei ya chini kwa mazao yake. hapa CHADEMA imapata kura za wasiolima ambao ni 30% na kukosa 70% ya wakulima.
SABA - Unafiki, Mungu hasimami na wanafiki hata siku moja.
Nitaendela mkija kujadili...