Kwa tamko hili, Bodaboda mnawaibia waajiri wenu

Kwa tamko hili, Bodaboda mnawaibia waajiri wenu

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Rasmi tena bila kupepesa macho Bodaboda nchi nzima kupitia wawakilishi wenu mmeutangazia Umma wa Watanzania kwamba katika shughuli zenu mpya za "Uafisa usafirishaji" mnapata Tshs. 800,000+ kwa mwezi.

Hii ni wastani wa 200,000 kwa kila wiki. Hapa Mafinga nilipo nawajua wamiliki wengi wa Bodaboda walioajiri vijana kwa rejesho la 40000-50000 kwa wiki. Yaani mwenye kiwanda anapata robo ya faida inayotengenezwa na mfanyakazi?

Niwasihi wamiliki wote wa Bodaboda nchini waanze kudai rejesho la angalau 100,000 kwa wiki ili kugawana faida na watumishi wao ambao kwa sasa kipato chao kinawazidi Walimu na Polisi wengi nchini.
 
Itakuwaje nyie mpate laki 8 kwa wiki halafu sisi wenye vyombo tupate laki2?
 
Back
Top Bottom