Sina nia ya kuwadharau wale wenye elimu ya Darasa la Saba ila ninaandika haya kwa kuzingatia nafasi ya uwakilishi wa Jimbo na unyeti wa nafasi hii. Dunia/Tanzania ya leo siyo ile ya miaka ya 60s. Tunahitaji mabadiliko makubwa katika nyanja zote ikiwemo katika nafasi za ubunge.
Mbunge ni mtu muhimu sana katika eneo analoliwakilisha na ndiyo maana anaheshimika na kulipwa mamilioni ya pesa kutoka na unyeti wa kazi anayoifanya au nafasi aliyonayo.
Mbunge anayeongoza Jimbo lenye kata 30 anakuwa na elimu ya Darasa la Saba, ila afisa mtendaji wa kata anayeongoza kata moja anatakiwa angalau awe na Diploma/shahada. Hiki Ni kichekesho sana na Tanzania inatakiwa tubadilike ili kuendana na uhalisia wa sasa. Tumebaki nyuma sana katika mambo mbalimbali likiwemo hili la kuwa na wawakilishi ambao uwezo wao na nafasi zao haviendani.