Kwa Tanzania kazi ya upolisi ni kazi yenye changamoto sana

Kwa Tanzania kazi ya upolisi ni kazi yenye changamoto sana

The unpaid Seller

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2019
Posts
2,113
Reaction score
6,251
May all souls find enlightenment,

Kama unaupenda uzao wako na ungependa kuwaepusha na hekaheka kamwe usimpeleke mtoto wako upolisi.

Kwa uzoefu wetu sote tunajua jinsi baadhi ya Polisi kuwa ni watu wa dhuluma, uonevu na unyama wa kutisha unaweza kusema mtu fulani mtoto wako au ndugu ni mwema kwahiyo hata akijiunga na upolisi atatenda tofauti, hakika unajidanganya.

Uovu kutoka jeshi la upolisi sio jambo la mtu binafsi ni mfumo mzima umeoza, kuanzia ndani mpaka nje na kibaya zaidi wao wanafuata amri, hawahoji na wala hawana choice ni kupokea maagizo na kuyatekeleza hata kama dhairi ni uonevu na unyama wa kutisha kiasi gani.

Na kuhakikisha polisi wanakua watiifu kufanya unyama na wasihoji ndio maana wanachaguliwa wengi waliofeli, unadhani ni kwanini?

Licha ya kutumiwa kwa kazi chafu sana lakini hawathaminiwi, huishi kwenye vinyumba vya vya kwota vya mabati lakini wakivaa nguo zao wakapanda ndani ya defenda zao hujiona kama wao ndio wao masikini wangejua mshahara wao na haufiki hata nusu ya posho ya kikao cha watawala wanaowatumia.

Hatma ya hawa polisi siku zote hua ni majanga WENGI wanastaafu wakiwa masikini na magojwa ya stroke huwapiga sana (Kuna thread humu inazungumzia takwimu za kutisha za polisi wastaafu wanaougua stroke).
 
Nyongo imetemwa na Mtu amekuwa na amani.
Nani aliyesema Maisha ni Mwalimu asiyekosea na hayana kanuni?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Kwahiyo nini kifanyike?
Kwa sasa ni kuepusha UZAO WAKO na laana inayoambatana na upolisi, pili kama taifa yatupasa kufanya mapitio ya mifumo yetu ya law enforcement lakini kwa uafrika wetu usitegemee hili kutokea maana uovu wa mapolisi UNAWANUFAISHA SANA WATAWALA
 
Kwa sasa ni kuepusha UZAO WAKO na laana inayoambatana na upolisi, pili kama taifa yatupasa kufanya mapitio ya mifumo yetu ya law enforcement lakini kwa uafrika wetu usitegemee hili kutokea maana uovu wa mapolisi UNAWANUFAISHA SANA WATAWALA
Mi ndo naomba kazi huko japo sijapata ila zikitoka naomba tena
 
Back
Top Bottom