Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Kwa hali inayoendelea hivi sasa nchini, Kwa tuhuma za matukio kadhaa ya uvunjifu wa sheria, madai ya kupotezwa Kwa watu kadhaa, na kudaiwa kuuawa Kwa raia wasio na hatia.
Matukio yote haya, yanadaiwa kuhusishwa na Jeshi letu la Polisi, kuwa ndiyo watekelazaji wakubwa, Kwa hiyo inalazimu hivi sasa, Jeshi hilo la Polisi nchini, likawa na chombo kingine kikawa ni "overseer" wake wa namna Jeshi hilo linavyotekeleza wajibu wake, kama ni Kwa mujibu wa Katiba ya nchi, vile vile ni Kwa mujibu wa miongozo, kama ilivyo Kwenye PGO yao wenyewe ya Jeshi la Polisi.
Siyo Siri tena kuwa Jeshi hilo la Polisi, linafanya mambo mengi ya ya hovyo, likiamini kuwa hakuna chombo kingine ambacho ni "overseer" wa utendaji wake
Wananchi tunajua wazi kuwa wajibu namba Moja wa Jeshi letu la Polisi ni kutulinda sisi raia na Mali zetu.
Wanachofanya Jeshi i letu la Polisi ni kinyume Cha hivyo. Kwa ajili wenyewe ndiyo wamekuwa kinara wa kuvunja kanuni hiyo!
Kuna matukiu kadhaa yanatokea nchini ya uhalifu, wakati wananchi tukilituhumu Jeshi la Polisi kuwa ndiyo waliotekeleza uhalifu huo, wakati huo huo Jedhi hilo linatuhakikishia kuwa lenyewe ndilo litakalofanya uchunguzi na ikibainika kuwa uhalifu Kwa wahusika kama wametoka Kwenye Jeshi hilo, litawagfikisha mahakamani wahusika!
Hivi inakuwaje "suspect" mkubwa akawa ndiye atakayeendesha uchunguzi na ikibainika kuwa kosa limefanyika, ndipo ajifikishe mahakamani??
Kuna tatizo kubwa sana Kwenye Katiba yetu ya nchi, Kwa kulifanya Jeshi letu la Polisi, kutokuwa na chombo kinachowachunguza wenyewe wakifanya makosa mbalimbali
Kuliweka Jeshi la Polisi chini ya chombo kingine, ambacho ni "overseer" wake ni mfumo ambao unatumika Kwenye nchi nyingi Duniani hivi sasa
Kama hali ikiendelea hivi ya haki kutotendeka nchini na Jeshi la Polisi likiwa ndiyo watuhumiwa wakubwa wa kutotendeka haki hiyo, ninaiona hatari kubwa ya kutokea machafuko nchini Kwa siku za mbeleni!😗
Mungu ibariki Tanzania
Pia soma:Napendekeza Jeshi la Polisi kusukwa upya kuondoa tuhuma za mauaji zinazolikabili mara kwa mara