Kwa Tukio lililomtokea Mama yangu 2009, Nimetokea kuuheshimu sana Ukristo na Wakristo wote

Huyo mtumishi atakuwa ni Mwl Christopher Mwakasege.

Nashukuru kwa ushuhuda🙏🙏🙏

Mungu wetu ni wa upendo. Anawapenda wote na anatamani kujifunua kwa kila kiumbe.

Anawapenda wote, wewe ukiwemo. Anakufahamu kwa jina lako na anakupenda vilivyo.

Nashukuru sana kwa ushuhuda🙏🙏🙏
 
Anyway nimeingia Jukwaa linaloruhusu kuandika uwongo. Samahani natoka.

Hakuna mtu mwenye akili yake anaeeza kuandika maradhi ya mama yake hata kama anatumia fake ID
Hajaandika maradhi, amemtumkuza Mungu kwa kile alichokifanya. Madaktari wana falsafa yao maarufu: "Sisi tunatibu, Mungu anaponya"
 
Uponyaji wa Imani unafanyika Kwa Imani. Sasa anaendaji Ocean road Kwa wagonjwa ambao hawajawa na Imani hiyo????
Hata Yesu alishindwa kuwaponya watu wa nyumbani kwao Nazareth kwa sababu ya kutokuamini kwao. Alitamani kuwafanyia miujuza mikubwa lakini wakamfunga breki kwa kutokuamini kwao.
 
Mbona na Wakatoliki nao siku hizi wanombea wagonjwa?

Unawafahamu wana Karismstik wa Katoliki?
1. Wanakemea mapepo!
2. Wanawaombea wagonjwa!
 
Miujiza ya Mwenyezi Mungu ipo na inafanyika kila iitwapo leo, kikubwa ni kuamini kwa moyo mmoja. Nb Mungu azidi kumtia nguvu mtumishi wake. Mwl. Christopher Mwakasege
Amina!

Kupitia huduma ya Mwl Mwakasege watu wengi sana mimi nikiwemo wamesaidika sana.
 
Umesimulia tukio vizuri mno kiasi Cha kuinua hata Imani inayolega lega utafikiri nilikuwa naona Kila unachoeleza
Mungu aendelee kumtunza mama yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…