Huu uzi unaletewa mzaha lakini ungekuws serious unaweza kusaidia watu.
Wengi wanapata 0 form IV au VI halafu wanachizi kabisa, wengine mpaka wanakunywa sumu. Kwa waliowahi kupata 0, share experience.
Mimi nitashare ya mwalimu wangu chuo
Alipiga 3 akiwa form 4, form Six akapiga 0. Anakwambia home kulikuwa kubaya kuliko maelezo. Bahati nzuri kuna ndugu yake alikuwa chuo, akamwambia njoo ufanye certificate ya IT. Na jamaa alikuwa interest na computers. Akatoboa vizuri certificate, akaenda Diploma akapiga vizuri. Akaanza Degree ya Computer Science, jamaa aliongoza course nzima. Chuo kikampeleka Finland kufanya masters na ajira akapata. Leo ni Networking guru, PHD, na mwalimu mzuri sana.