Kwa tuliotahiliwa bila ganzi tu.

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,959
Reaction score
24,935
Kwa wale wote tuliotahiliwa(kuingia jando) bila ganzi tukutane hapa .

Vipi maumivu yake wakuu? Je wewe uliambiwa nini siku ile waliyokuja kukutahili kama kukutoa hofu au kukudanganya usiogope.

Binafsi nilidanganywa kununuliwa viatu si unajua enzi hizo viatu vilikuwa adimu sana wamiliki wake ilikuwa watoto wa walimu au wafanyakazi tu wa serikari.

Basi siku hiyo nilikuwa zangu nacheza Mara pap nikaitwa nyumbani nilijua tu naitiwa kupiga msosi kumbe naenda kutailiwa.

Asee maumivu niliyoyapata wakati natailiwa si mchezo nilibanwa kila kona ili nisikurupuke nashukuru nilifanyiwa fresh na sasa mi kidume kitaani.

Vipi upande wenu wakuu.
 
Mimi nilidanganywa kununuliwa baiskeli looh maumivu yake
 
Hahaha wapuuzi walinidanganya nijifiche mgongoni (nlibebwa Kama mtoto mdogo) eti nitang'atwa na nyuki, nakuja kushushwa na mtama juu mpaka chini... Sijatulia ngariba ashalamba govi langu, wakanituliza kwa madafu ila daaaah hata sikufurahia kabisa madafu yenyewe
 
Mi nilitahiriwa maumivu yaleee hasa nikitaka kukojoa duuuu halafu kichwa kilibaki kikubwa lol....acha tuuu
 
Duuuuh Umenikumbusha mbali sana.. Mimi nilijua kuwa naenda kukatwa, tulikua kama watano hivi, kufika kule nikasikia wenzangu wanalia, Mi nilikua wa mwisho..

Nilikua nimevaa kaptula ya kadeti na mkanda, ngariba akawa ananivua mkanda nakataa, mara akachomoa kisu, nikatulia, nikafumba macho akalegeza mkanda, sikikusikia maumivu wakati anakata, maumivu ni wakati anachuna ile ngozi nyeupe katika kichwa.. Ila sikulia, sema mangaliba wapo shapu sana..

Jandoni raha sana, tuliokaa porini tumefurahia maisha, una kalili nyimbo zaid ya Mia..

Unadanganywa siku ya mwisho anakuja fisi na spoku ya moto, kuongeza Tundu la mkojo, unaogopa sana.

Ukiwa Jandoni, akija mtu aliyetailiwa kabla yako unatakiwa kumwamkia hata kama umemzidi umri, vinginevyo utakula adhabu za kufa Mtu
 
Mshua aliongea bila chenga kua lazima nikatahiriwe chaka uko kwenye chimbuko lao kwa kua mimi ndio mtoto wake wa kwanza na pia miaka ile ilikua ni familia chache wanatahiri hosp,siku ikifika nikapelekwa shamba nikakutana na kundi la vijana kama mia tayari kwenda jandoni duh yule ngariba shababi haswaaa maana tulikua foleni ndefu ila ukifika unabiduliwa hata sikuelewa kilochofuata ni maumivu makali na tulikaa porini almost miezi 2 ila namshukuru mshua sijutii kukaa porini mpaka leo yapo mengi kule nadhani wenzangu mnayakumbuka.
 
Mi hata sikumbuki nimekuta dushe limekatwa, kuna siku hv hv mkubwa nipo kama 23 yrs nilimuuliza mama akaniambia ivi wewe una kichaaa unaniletea ushenz unataka nilirudishe gozi lako, mpk leo sijui chochote
 
Hahaha umeua mkuu.
 
Mimi nakumbuka tulikuwa wawili mimi namdogo wangu wakunifata,walituweka kwenye madishi ya maji hili dushee zilainike mzee kilichofata hapo ni kutinduliwa govi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…