brokenagges
Member
- Sep 29, 2022
- 58
- 33
Nipo maeneo ya Arusha mjini, ninasikitishwa sana na hali niliyoiona maeneo ya barabara ya Sokoine jirani na hospital ya AICC. Eneo hili ni mahali kilipo chuo cha utalii cha Tropical Institute.
Ukataji miti unaofanyika hapo barabarani eneo la nje ya chuo kwa sababu ya kupasafisha ili mgahawa unaojengwa ndani ya eneo hilo uonekene, eneo hili la hii barabara ukitembea kuna mandhari zuri sana kwa sababu ya miti ambayo imeoteshwa kwa mpangilio pembezoni mwa barabara kwa wanaopafahamu kupitia kibo palace hotel.
Soko la Madini Arusha hadi kufika maeneo ya round about ya impala na hii miti ni mikubwa na imekuwepo miaka yote, sasa cha ajabu ni kwamba wenye biashara ya mgahawa hapo kwa sababu pengine ya kutokufikiri vizuri wameamua kukata hiyo miti ili tu kwamba mgahawa uonekane na bila kujali mazingira wala kufikiri kwamba hiyo miti thamani yake ilikuwa kubwa kiasi gani.
Nikawa najiuliza ni mamlaka gani zenye kutoa kibali kama hicho na nani. Wanaohusika kusimami mazingira wanakuwa wako wapi wakati haya yakifanyika? Naomba wanaohusika na mazingira wajitahidi bila kujali ushawishi wa pesa watunze mazingira mti haukui kwa miaka miwili wala mitatu mti unakuwa hadi miaka hamsini na hata zaidi na haifai kufanya mji jangwa kwa sababu ya tamaa ndogondogo.
Elimu itolewe watu wawlewe maana ya mazingira ili wayatunze.