Kwa ubunifu huu Platnumz ataendelea kutamba kwa miaka kadhaa ijayo

Ngonepi

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2013
Posts
1,872
Reaction score
1,207
Licha ya kutaka tu mziki mzuri lakini tunapenda vionjo vingine pia kutoka kwa Mwanamuziki. Msanii/Mwanamuziki/Mburudishaji yafaa kuishi kisanii kama kazi uliyochagua inavyokutaka na si kuleta mambo ya faragha au kujifanya mwenye staha saana (mradi usivunje sheria).

*Fashion, namna anavyovaa.
*Mwonekano, Asikwambie mtu mwonekano hasa body unasaidia sana kuigusa hadhira.
*Kujithaminisha, jifanye ghali sio wa rahisirahisi.
*Dance/Cheza, Hili hadhira inafurahishwa nalo sana!
*Life style ya kisanii.
*Mbinu kali katika kutafuta na kuyaona masoko ya muziki/bidhaa yako.

Jamaa ni msanii aliyekamilika kwa ninavyomtazama, anajua sana kizazi hiki kinataka nini kutoka kwa msanii/mburudishaji na anatupatia kwa kweli.

Hili limefanya karibu Media zote hasa hizi Online kujikuta zinahitaji mno habari za Diamond ili kujitengenezea wafuatiliaji wa media zao.

Yaani kwa sasa media isiyoandika au kuzungumzia Diamond na WCB kwa ujumla inajichelewesha yenyewe!!

Tukubali au tukatae lakini Diamond anabaki kuwa ndie alama au dira kwa upande wa burudani hasa ya kizazi kipya hapa Tanzania. Ni vile tu Sisi weusi tumeumbwa kuchukia wanaofanikiwa kuliko kujifunza kupitia kwao!

Big up Platnumz.
 
Hakuna la kuongeza, umeandika yote. Diamond Platnumz ni a full package artist.

Jamaa anajua kuji-brand, na maisha yake kwa asilimia kubwa yapo public na hii inamfanya aongeze thamani na mashabiki maana ukiwa staa kila kitu hakipaswi kuwa private, mashabiki wanataka kuyajua maisha yako vizuri sasa ukijifisha kama kobe unakuwa kama naniiiii!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa,kwa sasa hapa Tanzania Icon ya bongoflava ni Diamond, inshort jamaa ni package iliyokamilika.Lakini tusisahau jamaa ananidhamu kubwa sana na wafanyakazi wake husasan akiwa nao mbele ya media the way anavyo taniana nao,kuongea nao kama n mkubwa wake anamwita braza hii inamfanya hata wafanyakazi wazidi kujituma.

Angalia jinsi anavyoishi na managers wake bila bifu ndio maana kila siku wanaumiza vichwa ili wazidi kum-brand
 
Diamond ni timu ya watu ipo nyuma yake.. lazima afanikiwe tu..

Diamond ameamua kula na watu. Sio mchoyo..

Hebu waza tu wamekaa kikao watu 50 ,babu tale, sallam, fela , diamond, producer lizer, s2 kizzy, director kenny, zuchu, ray vanny, mose iyobo na wengine kibao wanapanga jambo.. lazima liwe zuri tu..

Wasanii wengine ni wabinafsi.. wanaona wakiweka timu kubwa hawatatajirika.. sasa wanabana matumizi kwa kufanya kila kitu wenyewe.. wazo la mtu mmoja haliwezi shindana na wazo la watu watano au kumi
 
Nakubali!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diamond ataendelea kushikilia industry ya music jamaa anajua Nini kinaitajika na kwa wakati upi hakuna mtu aliyetegemea watakuja idea ya Quarantine wakati wasanii wengi wamejikita kuimba Corona na madhara yake wao wakaja kitofauti na wamekuja kwa beat ya hip-hop sio ya kuimba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…