Kwa Udhamini wa Mkutano wa Kimataifa wa Connect2Connect Africa, Helios Towers, Yazidi Kuing'arisha Tanzania, Kitaifa na Kimataifa, Yastahili Pongezi.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Kampuni ya Helios Towers, inayoongoza kwa miundombinu ya mawasiliano kwa njia ya minara, imepongezwa kwa kuing’arisha Tanzania kitaifa, Afrika na kimataifa, kulikopelekea mkutano wa 8 wa Connect 2 Connect (C2C) Afrika 2024, kuja kufanyikia Tanzania, Hellios akiwa ndie mdhamini mkuu wa mkutano huo ulianza jana katika Hoteli ya Gran Melia jijini Arusha na unaratibiwa na kampuni ya Extensia Limited, kwa ushirikiano na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Helios Towers Tanzania na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki ya Afrika, Gwakisa Stadi, amesema Mkutano wa C2C Afrika ni tukio la kipekee katika sekta ya mawasiliano, likiwaleta pamoja wakurugenzi waandamizi, na viongozi wa katika sekta ya mawasiliano kujadili, fursa, na changamoto zinazokabili sekta ya tehama barani Afrika.

Gwakisa Stadi, amesema mkutano wa mwaka huu utaangalia mada kama vile mustakabali wa miundombinu ya mitandao, uimara wa kidijitali, mifumo endelevu, na mitandao ya broadband, ambayo yote ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa kidijitali wa bara la Afrika.

Gwakisa Stadi alisema: "Kama mdhamini mkuu wa Mkutano wa C2C Afrika kwa mwaka huu, kampuni ya Helios Towers inajivunia kuchangia katika mazungumzo yatakayounda mustakabali wa uunganishaji barani Afrika. Tunaamini kuwa miundombinu ya mawasiliano yenye nguvu, endelevu, na inayoweza kupanuka ni ufunguo wa kufungua uwezo wa kidijitali wa kanda hii. Natarajia kushirikiana na viongozi wenzangu wa sekta tunapofanya kazi pamoja ili kuendeleza mabadiliko ya kidijitali na kuunda matokeo chanya ya muda mrefu katika eneo la Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara.”

Mkutano wa C2C Afrika 2024 umeshirikisha washiriki zaidi ya 300, ikiwa ni pamoja na wawakilishi kutoka kwa makampuni ya simu (MNOs), wawakilishi wa makampuni ya Fibre (FNOs), kampuni mbalimbali za miundombinu, waangalizi, na wadau wengine muhimu katika mfumo wa Tehama katika bara la Afrika. Washiriki wote watapata fursa ya kuungana, kushiriki katika majadiliano na kubadilishana mawazo ya kuongeza fursa za kuimarisha mandhari ya kidijitali kote barani.

Helios Towers ni kampuni inayoongoza katika miundombinu ya mawasiliano yenye idadi kubwa zaidi ya minara barani Afrika na Mashariki ya Kati. Kampuni hii inaratibu ufanisi wa kushirikiana miundombinu na makumpuni ya mitandao ya simu (MNO) ili kufanikisha upatikanaji wa mitandao ya simu kwa haraka, kwa gharama nafuu na kuzingatia utunzaji wa mazingira kwa kupunguza matumizi ya alama za kaboni (carbon footprint). Hii kwa upande wake inasaidia upanuzi na ubora wa mawasiliano kwa njia ya simu, ikichochea maendeleo endelevu katika masoko yake.
Kujua zaidi kuhusu Helios Towers na huu Mkutano wa Connect2Connect karibu
View: https://youtu.be/JkTyaH6xrtk?si=-mfEt9X9GPhv38yi
Gwakisa.jpg
Gwakisa 1.jpg
Gwakisa 3.jpg
Gwakisa Stadi, Mkurugenzi Mtendaji wa Helios Towers Tanzania na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashari...png

Paskali.
 
Safi sana Helios Tower....Hivi Bado wapo Oysterbay au washaondoka pale?
 
Back
Top Bottom