MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Nimejaribu kuangalia ile mobilization iliyofanywa na wasanii kule nchini Nigeria kina Davido na wenzake wakiandamana kuomba kile kikosi maalum cha Polisi kinachotesa Raia kivunjwe na hatimaye mamlaka zimekivunja. Huku Bongo Wasanii wa kizazi kipya kina Diamond na kundi lake wanakata mauno kwenye kampeni za CCM wanaomba kura. Yaani hopeless kabisa na aibu.
Kwa uelewa wangu mimi ni kwamba duniani kote vyama vya siasa huwa na wasanii maalum kutumbuiza wakati wa kampeni badala ya kutumia wasanii maarufu ambao wanajua hawawezi kuitikia maombi yao kwa kuogopa kugawa mashabiki. Hivi leo unafikiri mwanachama Kindakindaki wa CHADEMA au ACT atampenda Alli Kiba au Diamond Platnumz?
Ukiona hivi ujue ni umaskini ndiyo umekithiri, msanii anayejitambua mwenye pesa zake hawezi kufanya kazi za siasa kwanza hana muda huo labda aamue kugombea yeye. Tuna wasanii 90% darasa la saba na form four failures ambao hawana skills za kuwafikisha mbali kusimama wenyewe. Maarifa ya kufikiria kuwa siasa ni tukio la Msimu hawana. Mtu akipewa mkono na Rais kesho kichwa kimevimba.
Diamond angekuwa na pesa asingehangaika na kampeni za CCM kulipwa pesa za madafu. Wengine wanakopwa na wapo wanaolipwa kiduchu sana.