Kwa ufundishaji huu,matokeo ya mitihani yatafutwa kila mwaka

Kwa ufundishaji huu,matokeo ya mitihani yatafutwa kila mwaka

kyaseni

Member
Joined
Jan 11, 2013
Posts
15
Reaction score
1
IKIWA matatizo ya walimu hayatashughulikiwa ipasavyo ikiwemo kupata walimu wenye viwango vinavyokubalika
ninahakika matokeo ya miyihani yatakuwa yakifuta kila mwaka wala siyo kwa kidato cha nne pekee bali hata kwa kidato cha pili pengine hata shule za msingi,ukiondoa wale wa kidato cha sita ambao wameshushiwa kiwango cha ufaulu.

Nasema hayo siyo kuwa nafurahia hali hiyo la hasha ila ni ukweli usiopingika kwani ninaishi karibu na shule ya Sekondari ya kata inayofahamika kwajina la King'ongo Sekondari,nawasikitikia wazazi wanaolipa ada kwenye shule hiyo kwa lengo la kuhakikisha watoto wao wanapata elimu.

Simaanishi kuwa wasilipe bali watenge muda wa kufuatilia ili kujua kama watoto wao wanafundishwa na walimu wanaofahamu kazi zao kikamilifu, sina maana mbaya kwa walimu wa shule hiyo ila kuna baadhi yenu wasiofahamu wanachokifanya.

Hili jambo haliwezekani kwa mwalimu wa kiingereza anayefundisha kidato cha pili kuwafundisha wanafunzi mambo ambayo walipaswa kufundishwa wakiwa darasa la 1 na 2 ama middle class kwa shule za msingi wanazotumia lugha hiyo,kumfundisha mwanafunzi kazi anayoifaya polisi,daktari,fundi bomba,askari wa usalama barabarani siyo uungwana pia hayalingani na yale yanayomkabili mwanafunzi wa kidato cha pili.

Badala ya mwalimu kufundisha tenses,gramma na mambo mengine ambayo ni magumu kutokana na lugha hiyo kuwa ngeni kwa watanzania wengi anafundisha mambo yasiyokuwa na manufaa wala hayatawasaidia kwenye mtihani unaowakabili hiyo ni hatari kwani matokeo ya kidato cha pili yatafutwa ikiwa wanafunzi wengi watafeli.

WIZARA ZINGATIENI WALIMU MUNAOWATUMA KUFUNDISHA.







u
 
Syllabus ya form two kiingereza inasemaje?
 
Back
Top Bottom