Kwa ufupi Hayati Magufuli aliwachukia watumishi wa umma

Mlalamikaji daily

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2014
Posts
744
Reaction score
1,621
Kwa ufupi sana JPM alitamani kuona Wafanyakazi nchi hii wanaishi kama mizuka, mizimu au mazombi.. hakuna ajuae ni kosa Gani haswa aliwahi kufanyiwa na watumishi wa nchi hii, yapo mambo ambayo mama amejitahidi angalau kuyarudisha lakini mengine inabidi mchakato au hata hekima tu, ngoja niwaonyeshe Machache,

1. Kupandisha Madaraja , kwa Mfano wafanyakazi walioajiriwa mwaka 2014, haikujulikana ni LINI, wangepanda Madaraja! Imagine Miaka 7, na hatimaye wakaja kupanda mwaka 2021! Baada ya mama kuingia madarakani! Just imagine

2. Nyongeza za kawaida za Kila mwaka ambazo zipo kisheria kabisa yeye alifuta! Tena Bila shaka hakutaka kusikia, haijafahamika mara moja ni kwanini!

3. Kazi maalum kwa walimu Mfano (kusahihisha mitihan ya taifa)
Walimu waliokuwa wakifanya Kazi iyo kabla ya JPM kuingia madarakani, mbali na kwamba walilipwa vizuri pia walikula chakula kizuri, lakini pia waandaaji walifanya kama kuwamotisha walimu kwa kuwapa kama utalii wa ndani, maana yule wa kigoma angeenda Tanga wa Tanga akaenda Tabora huko n.k...

Hii iliwafanya baadhi ya watu kufurahia na angalau kubadilisha mazingira!
Sasa Mzee baba alivyoingia akapiga marufuku akisema wa Tabora abaki Tabora na WA Mwanza abaki mwanza! Hakuishia hapo na malipo akapunguza! Akidai walimu hiyo ni kazi Yao, hivyo ikibidi wasilipwe chochote! Na Sasa kuanzia pale kazi ikawa Haina morali kwani kazi kubwa, malipo kidogo na masimango juu.

Mpaka tunakwenda mitamboni haikujulikana sababu haswa kwanini Mzee baba aliwachukia wafanyakazi kiasi hiki.
 
Alikuchukia wewe kwa kuwa ulikuwa na cheti fake lakini sisi watumishi wa vyeti original hatukuwa na shida naye kabisa.
 
Back
Top Bottom