Kwa Ufupi: Jitihada za Kuikwepa ICC zinaendelea....

Mkuu Mzee Mwanakijiji, be optimistic than pessimist

P
Unawezaje kuwa optimistic kwa jambo la wazi lenye formula kabisa?

Tume ya Chande watu walitoa matokeo tangu mwanzo wa kuundwa kwake.

Na hii wametoa matokeo yatakavyokuwa kwa sababu formula ya jambo hili ipo wazi.

Je wewe mkuu wadhani tume inaweza kumuita na kumhoji Rais ambaye kikatiba na kiuhalisia ndiye aliyaamuru majeshi kuuwa raia?

Na asingelikuwa ni yeye wote waliopoka madaraka yake wangekuwa korokoroni saa hii.

Kwa hiyo matumaini yako tume hii kutenda maajabu kinyume na formula iliyopo?
 
Wanajaribu kupunguza machungu ya wananchi na kuonyesh mataifa ya nje kuwa bado serikali inawajali wananchi wake
 
Ili kukwepa mkono wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) viongozi wa Tanzania walitakiwa waanzishe na kuleta mashtaka dhidi ya wahusika wa mauaji ya mamia ya Watanzania Octoba 29 mwaka jana.
Shida niliyonayo ni kuendelea kushikilia hiyo ICC. Sijui kwa nini bado kuna watu wanategemea kuwepo uhusika wa ICC katika swala la Tanzania.
Kuna mahali popote walipoonyesha kuwa bado wanaendelea kulitazama swala hilo?

Haya matumaini yanatokana na nini?

Samia anao mpango wake wa kumhakikishia kuwa atamaliza ngwe yake hapo 2030, kama waTanzania hawatastuka na kumkatisha ndoto zake za kipuuzi
 
Why should he be? At least give him some reason
 
Mipango ya kumng'oa imekamilika
 
Na kuna uwezekano kadiri muda unavyokwenda ndivyo ushahidi wowote uliopo unavyozidi kupunguzwa nguvu. Msidharau hizi hatua zinazochukuliwa. Kete inasukumwa kwa umakini sana.
Duh!
'Strategist', unaona kuna "kete inayosukumwa kiumakini" hapa!

Kama tutaanza kuona "umakini" katika hili; basi hatujui umakini ni kitu gani.

Ukisema lengo ni kupoteza muda, naweza kukubaliana na wewe, kuliko kuwepo na umakini kwenye hatua hii.
 
Kama bado hujafika umri wa miaka 50, nadhani unaweza kuwa umechanganyikiwa.

Huna majibu na bado huna matumaini na hivyo kazi yako ni kukaza fuvu kwa matumaini ya wengine
 
Kama bado hujafika umri wa miaka 50, nadhani unaweza kuwa umechanganyikiwa.

Huna majibu na bado huna matumaini na hivyo kazi yako ni kukaza fuvu kwa matumaini ya wengine
Hakuna aliyechanganyikiwa katika hili la Samia na uovu wake kama yeye mwenyewe na watu kama wewe mnaomtegemea kama mifugo wake.

Samia anaishi kwa muda wa kuazima tu sasa hivi.
 
Kwa hiyo kwa kifupi tunasema bado tena wamepaisha penalti
 
Je wewe mkuu wadhani tume inaweza kumuita na kumhoji Rais ambaye kikatiba na kiuhalisia ndiye aliyaamuru majeshi kuuwa raia?
Mkuu, 'Sakasaka Mao'; naomba usinione mjingamjinga hivi, au hata mpumbavu kabisa juu ya hili la "majeshi kuua raia"
Ukweli ni kwamba sina uhakika wa haya "majeshi" kushiriki katika mauaji.

Picha zooote nilizowahi kuziona za watu waliokuwa mitaani na silaha siku hizo sijaona hata moja iliyoonyesha kwa uhakika kwamba ni POLISI; au Askari wa Jeshi la wananchi la Tanzania.

Hata mitaani nilikokuwa siku hizo sikuwahi kumwona askari polisi yeyote na silaha; au mwanajeshi na silaha, huko mitaani.

Huu ushiriki wa majeshi kuua waTanzania uhakika wake ni upi?

Siku hizo walipewa amri ya kutojitokeza miraani wakiwa kwenye nguo zao rasmi?

Je, hakuna uwezekano kwamba hawa watu waliohusika kwenye mauaji hawahusiki kabisa na jeshi la polisi au JWTZ?

Hawawezi kuwa wameandaliwa mapema kutimiza lengo hili; halafu na kuwashirikisha polisi kinamna tu?

Kama kuna ushahidi wowote unaobainisha wazi kuwa polisi na jeshi la wananchi walihusika; mbali ya matamko tu, naomba tafadhali nifahamishwe' ili ujinga/upumbavu wangu ukome.
 
Hili jambo la kila kukicha wanateua tume wakati mambo yote yako wazi ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi kwani nikupeana ulaji tu kwa wajumbe. Hakuna jipya litakalotolewa zaidi ya kutunga tamthilia yenye seasons nyingi tu.
 

Wanajaribu kubuy time na kuhamisha mgoli.
 
Ahaa!
Haupo mbali katika kufikiri.

Picha zilizoonekana siku hiyo waliobeba silaha ni watu mostly walivaa kiraia.

Katika department ya Polisi, kuna askari kanzu huvaa kiraia.

Polisi waliokuwa na silaha walionekana pia.

Wanajeshi walionekana hawana silaha walipokuwa kwenye magari.

Sisi tulio nje ya Dar tunaeleza namna tulivyokuwa tunaangalia kwa kupitia video clips.

Ninyi wa Dar mnaweza kuwa mashuhuda wazuri.

Hayo ya Polisi ama wanajeshi kuhusika ama kutohusika siioni mantiki yake wakati watu maelfu wameuawa kwa risasi za moto.

Issue kubwa hapa tunaogopa kumfunga paka kengele.

Wawe Kmkm, wawe ni Waganda kama ilivyosemwa ni rahisi sana kutekeleza mauaji hayo kama Polisi na majeshi walitaarifiwa toka ngazi za juu kuhusu kinachoendelea.

Jiulize, aliyewapa go ahead wauaji ni nani kama siyo Samia mwenyewe?

Wenye mandet ya kulinda raia wapi umeona wamewajibishwa?

Mtuhumiwa #1 ni Samia, hata maneno yapindishweje.

Hatujasikia tume aliyoiunda leo, hadidu zake za rejea zitakazowaongoza ni zipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…