Kwa Ufupi: Jitihada za Kuikwepa ICC zinaendelea....

Kwa Ufupi: Jitihada za Kuikwepa ICC zinaendelea....

Yaani tume ya kwanza iseme Kuna mauaji 518
Alafu ya pili ije ichunguze kama Kuna makosa ya jinai?
Sio kila kifo kina jinai, kwa vile askari walipewa order to shoot and kill, then waandamanaji waliouliwa kihalali ni waandamani wahalifu waliokuwa na silaha za moto, wakielekea Ikulu kumpindua Rais Samia na kupindua serikali na nchi, hawa ndio Rais Samia, aliowazungumzia kuwa wameuliwa kihalali for safeguarding the national security, hivyo wauaji waliokuwa wanatimiza wajibu wao kikamilifu wa kuilinda nchi na wamepongezwa, tena hawa watakuwa wameuliwa na JWTZ, jeshi likiua, baada ya kupokea amri, ni kama vita, hakuna kesi!,

Hivyo hii Tume Jinai inachunguza mauaji yote kwanza kwa kuthibisha hao waliotaka kupindua nchi wameuwawa kihalali, itaonyeshwa hizo silaha zao kama ushahidi na waliowawa wapi, kisha wale wengine wote waliouwawa pengine popote inje ya waandamanaji, polisi, jeshi na TISS, watawajibika!.
P
 
Shida niliyonayo ni kuendelea kushikilia hiyo ICC. Sijui kwa nini bado kuna watu wanategemea kuwepo uhusika wa ICC katika swala la Tanzania.
Kuna mahali popote walipoonyesha kuwa bado wanaendelea kulitazama swala hilo?

Haya matumaini yanatokana na nini?

Samia anao mpango wake wa kumhakikishia kuwa atamaliza ngwe yake hapo 2030, kama waTanzania hawatastuka na kumkatisha ndoto zake za kipuuzi
Mkuu, 'Sakasaka Mao'; naomba usinione mjingamjinga hivi, au hata mpumbavu kabisa juu ya hili la "majeshi kuua raia"
Ukweli ni kwamba sina uhakika wa haya "majeshi" kushiriki katika mauaji.

Picha zooote nilizowahi kuziona za watu waliokuwa mitaani na silaha siku hizo sijaona hata moja iliyoonyesha kwa uhakika kwamba ni POLISI; au Askari wa Jeshi la wananchi la Tanzania.

Hata mitaani nilikokuwa siku hizo sikuwahi kumwona askari polisi yeyote na silaha; au mwanajeshi na silaha, huko mitaani.

Huu ushiriki wa majeshi kuua waTanzania uhakika wake ni upi?

Siku hizo walipewa amri ya kutojitokeza miraani wakiwa kwenye nguo zao rasmi?

Je, hakuna uwezekano kwamba hawa watu waliohusika kwenye mauaji hawahusiki kabisa na jeshi la polisi au JWTZ?

Hawawezi kuwa wameandaliwa mapema kutimiza lengo hili; halafu na kuwashirikisha polisi kinamna tu?

Kama kuna ushahidi wowote unaobainisha wazi kuwa polisi na jeshi la wananchi walihusika; mbali ya matamko tu, naomba tafadhali nifahamishwe' ili ujinga/upumbavu wangu ukome.

Hilo la ICC kwa kweli haliondoi wajibu wetu sisi kuwawajibisha hawa watu. Binafsi naamini njia bora zaid sisi kuwashtaki hawa nakuwawajibisha nchini. Hatutaki wakimbie nchi ndipo ICC inapokuja. Mfano mzuri ni mashtaka ya ICC dhidi ya Durtete wa Ufilipino.
 
Lkn wewe ndo uliyewaaminisha watu humu kuwa ICC itaondoka na Samia soon
Ni wapi uliponisoma nikiandika maneno ya kipuuzi namna hiyo? Unajibishana na mtu ambaye maandishi yake yapo wazi humu JF, halafu hujui msimamo wake upoje juu ya jambo husika?

Nionyeshe popote nilipoandika maneno kama hayo unayonisakazia hapa!

Unapoingia JF kupoteza tu muda, matokeo yake ndiyo haya.

Kazi yako ni kuja kutetea tu Samia bila kujali uovu anaowafanyia waTanzania.
Sasa wewe utakuwa tofauti vipi na nguruwe anayefugwa na huyo huyo Samia?
 
Hilo la ICC kwa kweli haliondoi wajibu wetu sisi kuwawajibisha hawa watu. Binafsi naamini njia bora zaid sisi kuwashtaki hawa nakuwawajibisha nchini. Hatutaki wakimbie nchi ndipo ICC inapokuja. Mfano mzuri ni mashtaka ya ICC dhidi ya Durtete wa Ufilipino.
Kimsingi hapa nakubaliana na wewe, lakini pia katika juhudi zetu hizohizo, hata wakikimbia nchi kesi hiyo ndiyo itazidi kuwa imara zaidi kwetu kuwahusisha hao ICC wawatafute popote huko watakakokuwa, ambako hatuwezi kuwafikia.
 
Wanataka kina Maria Sarungi wawe convicted .Watamshtaki Maria na kutuma ombi Kenya kuwa anahitajika Tanzania kwa kesi ya jina. Mange pia et al.
Samia kamwe hawezi kuepuka kwa kushiriki kwake katika hatua zooote kuandaa mauaji hayo kabla hata ya siku yalipotokea mauaji.

Hatua zote alizotumia kubaki madarakani kwa mabavu zipo wazi tokea wakati wa kujiteua mwenyewe ndani ya CCM kuwa mgombea pekee wa chama hicho.
Ushahidi upo, hawezi kuufuta au kuuficha.
 
Nliona kwenye news huko Philippines icc warrant ya member of parliament hko
Jamaa alikamatwa na mtiti juu ulitokea 😄 akawa anatoka nduki vuta nikuvute
Mpaka wamdaka 😄

Ova
Na hapa kwetu, wahusika wote waliochangia kwa njia moja au nyingine iliyotufikisha kwenye hatua ya waTanzania kuuliwa kinyama vile ni lazima watambuliwe na kila mmoja wao awajibishwe kwa mchango wake husika.

Hili jambo haliwezi kuisha hivi hivi kwa Samia pekee kuwekwa jela au kaburini..
 
Nliona kwenye news huko Philippines icc warrant ya member of parliament hko
Jamaa alikamatwa na mtiti juu ulitokea 😄 akawa anatoka nduki vuta nikuvute
Mpaka wamdaka 😄

Ova
Hatari ,mambo ya sheria za kimataifa ni noma ,jamaa hawatanii wakikuingiza kwenye 18.
 
Ni wapi uliponisoma nikiandika maneno ya kipuuzi namna hiyo? Unajibishana na mtu ambaye maandishi yake yapo wazi humu JF, halafu hujui msimamo wake upoje juu ya jambo husika?

Nionyeshe popote nilipoandika maneno kama hayo unayonisakazia hapa!

Unapoingia JF kupoteza tu muda, matokeo yake ndiyo haya.

Kazi yako ni kuja kutetea tu Samia bila kujali uovu anaowafanyia waTanzania.
Sasa wewe utakuwa tofauti vipi na nguruwe anayefugwa na huyo huyo Samia?
Povu povu povu.
Yes, mi huingia humu kupoteza muda tu. Pole kwako ambaye kumbe kuingia humu kwako ni ajira!!
 
Ili kukwepa mkono wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) viongozi wa Tanzania walitakiwa waanzishe na kuleta mashtaka dhidi ya wahusika wa mauaji ya mamia ya Watanzania Octoba 29 mwaka jana.

Ili ICC isilete mashtaka dhidi ya watu fulani fulani ni lazima mchakato wa uchunguzi utosheleze viwango vya kimataifa vya upelelezi na kuonesha pasi ya shaka nani alihusika na ushahidi huo uwekwe hadharani na watu wakutwe na hatia.

Tume iliyoundwa leo nina mashaka kama itakidhi hili.

1. Haiwezi kumhoji Rais kutokana na kuhusika kwake

2. Haina mwakilishi wowote (kwa sasa) toka Ofisi ya AG au DPP ili watengeneze kesi unless hawa nao wakitoa ripoti yao watatuambia wanapendekeza DPP naye aanzishe uchunguzi mwingine!!

3. Ili mchakato wake uaminike ni lazima iwe huru kweli kumhoji na kumleta mbele ya Sheria mtu au kikundi cha watu wowote waliohusika na mauaji.


Jitihada hizi nazo zitafeli....
Screenshot_20260120-224356~2.png
 
Unawezaje kuwa optimistic kwa jambo la wazi lenye formula kabisa?

Tume ya Chande watu walitoa matokeo tangu mwanzo wa kuundwa kwake.

Na hii wametoa matokeo yatakavyokuwa kwa sababu formula ya jambo hili ipo wazi.

Je wewe mkuu wadhani tume inaweza kumuita na kumhoji Rais ambaye kikatiba na kiuhalisia ndiye aliyaamuru majeshi kuuwa raia?

Na asingelikuwa ni yeye wote waliopoka madaraka yake wangekuwa korokoroni saa hii.

Kwa hiyo matumaini yako tume hii kutenda maajabu kinyume na formula iliyopo?
Raisi aliunda tume kujichunguza mwenyewe.halafu ameunda tume kujichunguza mwenyewe.
Jaji wa wa mahakama ya rufani
Swali ni Moja tyu, nani alitoa amri ya jw kuvaa nguo za polisi na kuvaa nguo za polisi? Kwenda kuua watu mitaani? Kijana aliye uwawa salasala alishiriki maandamano? Wazazi wake walifikiwa na tume
 
Back
Top Bottom