Kwa Ufupi: Jitihada za Kuikwepa ICC zinaendelea....

Duh!
'Strategist', unaona kuna "kete inayosukumwa kiumakini" hapa!

Kama tutaanza kuona "umakini" katika hili; basi hatujui umakini ni kitu gani.

Ukisema lengo ni kupoteza muda, naweza kukubaliana na wewe, kuliko kuwepo na umakini kwenye hatua hii.

Justice delayed is justice denied. Halafu kumbuka kama ambavyo kuna mbinu za kisayansi za kutunza ushahidi zipo pia mbinu za kisayansi za kuharibu ushahidi. Kupoteza muda ni mbinu classic ambayo imewasaidia wengi sana hapa duniani kuchomoka kwenye kesi ngumu sana. Usidharau hii mbinu yao hawa watu hata kidogo.
 
Hayo ya Polisi ama wanajeshi kuhusika ama kutohusika siioni mantiki yake wakati watu maelfu wameuawa kwa risasi za moto.
Hapana.
Inamantiki sana hiyo kutofautisha waliohusika na mauaji.
Mwovu yeyote huko kwenye mamlaka anaweza kutengeneza kakikundi cha wauaji; halafu na kuwabebesha polisi/askari jeshi kuwa ndio walikuwa wanafuata amri waliyopewa na mamlaka. Hii ina maana kubwa sana.

Ndiyo maana sasa inaanza kujitokeza kuwepo na sintofahamu fulani hata huko kwa watenda maovu waliopo madarakani (nisome hapo juu kuhusu hiyo tume mpya kuchunguza waliohusika na mauaji)
Katika department ya Polisi, kuna askari kanzu huvaa kirai.

Sasa kama wanawajuwa na waliwapa silaha; hiyo tume inakwenda kumchunguza nani mwingine anayeshukiwa kuhusika na mauaji ya waTanzania?
Kwa hiyo hawa siku hiyo walipewa jukumu la kuua? Hii inaelzwa wapi katika taratibu za kazi za polisi?
Maana yake aliyeamua kuwatumia alikuwa na dhamira ya moja kwa moja kuua waTanzania; kwa sababu kazi ya hawa siyo ya kutuliza vurugu zozote, wao kazi yao ni kufanya uchunguzi na kubaini uhalifu unapotokea; siyo kutuliza au kuua wakati wa ghasia.
Jiulize, aliyewapa go ahead wauaji ni nani kama siyo Samia mwenyewe?

Wenye mandet ya kulinda raia wapi umeona wamewajibishwa?

Mtuhumiwa #1 ni Samia, hata maneno yapindishweje.
Samia anatumia tu nafasi kupoteza muda, akiwa na matumaini kwamba kwa aina fulani jambo hili litakwisha na kumwacha yeye na wahalifu wenzake waendelee kukaa madarakani kwa nguvu hadi 2030, au zaidi..

Atakuwa na bahati sana akiimaliza 2026 salama!
 
Justice delayed is justice denied. Halafu kumbuka kama ambavyo kuna mbinu za kisayansi za kutunza ushahidi zipo pia mbinu za kisayansi za kuharibu ushahidi.
Mkuu, 'Strategist', mimi ni mwanasayansi; maisha yangu yote yamekuwa ndani ya sayansi; sijawahi kuona sayansi ya namna hiyo; inayofuta uhalisia uliopatikana kisayansi. Hili nalisema kwa utimilifu kabisa. Kwa hiyo hapo hapawezi kuwepo na 'strategist' yoyote.

Sayansi ya kutengeneza matokeo FEKI haipo!

Na huo msemo wa "justice delayed....", kweli unaamini hivyo wewe au ni msemo tu unaotumiwa kuendeleza mjadala?
Ni nini maana ya 'delayed" wakati mwisho wa siku wahusika wanawajibishwa.

Unafikiri Samia ataepuka matokeo ya uovu wake kwa kuchelewesha tu haki kupatikana? Hii nayo tuiite "strategy"; kuchelewesha tu uwajibikaji wa wahusika?
 
The last kicks of the dying donkey.
 
Principally tunanunua muda kitu ambacho ni hatari zaidi sababu itafika muda tu haya mambo yatachunguzwa kwa haki. Ingekuwa mimi ningeruhusu tume huru alafu ningepambana kujiandaa na negotiations kwenye uwajibikaji. Ukichelewa ukafika muda nguvu huna huta negotiate wala kusikilizwa.

Hizi sarakasi ndio zina cement kimataifa kuamini hazikidhi standard na pressure ya tume huru haitokoma.
 
Bila kukosea majawabu yatakuja vizuri sana,baadhi ya askari watashtakiwa,baadhi ya wanasiasa watashtakiwa,itahusisha wa serekali,wa chadema na wote waliohusika kwa namna moja au nyingine,haiwezekani fujo kama zile zilipuke nchi nzima bila ya kuwepo ""special organizing task force""
 
Wananunua muda ili kuonyesha jamii za kimataifa kuna kitu kinafanyika, kupoteza ushaidi uliopo na kusahaulisha wananchi. Hakuna kitu hapa, it's just a netflix series.
 
Hiyo tume ni mkakati mwingine wa kulindana, kuwanufaisha wastaafu na kuwaficha wauaji.
LAKINI wakae wakijua kuwa zile damu za WaTanganyika hazitopotea bure!
 
Nasubiri majibu ya aliyetoa amri... Make muunda tume anajikoroga kama waliompa PhD zake.
Alafu Mkuu si watu walishakamatwa wakaachiwa au kuna WaTanganyika wenzetu wanatafutwa?
 
Yaani tume ya kwanza iseme Kuna mauaji 518
Alafu ya pili ije ichunguze kama Kuna makosa ya jinai?
 
Lkn wewe ndo uliyewaaminisha watu humu kuwa ICC itaondoka na Samia soon
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…