OCC Doctors
Senior Member
- Jul 20, 2018
- 113
- 172
Kipimo cha hesabu kamili ya damu (Full Blood Count) ambacho pia huitwa kipimo kamili cha damu (Complete Blood Count) au kipimo kinachotoa taswira kamili ya hali ya damu (Full Blood Picture) Ni kipimo cha uchunguzi wa damu ambacho hutumika kutoa taarifa muhimu kunako hali ya mgonjwa zinazosaidia katika utambuzi wa ugonjwa na usimamizi wa matabibu.
Kipimo hichi Hutumika kugundua magonjwa, upungufu wa damu, mchafuko wa damu, uchache wa chembechembe ndogo za damu (thrombocytopenia), maambukizi na saratani ya damu (leukaemia). Kipimo hichi hupima vipengele kadhaa vya seli za damu na hutoa taarifa muhimu kuhusu utengenezaji wa seli zote za damu na utendaji kazi wake.