Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Kwa Marekani wataalamu wa siasa za ndani kama Bob Bequn wanasema hivi "Siasa za Marekani zimegawanyika katika makundi makuu manne, kwanza ni siasa za Washington ambako umaarufu wa mtu kisiasa unaweza kuibuka kama uyoga na kuanguka ghafla kama jani kavu. Pili ni siasa za New York ambako siasa zake ni za kisanyansi zaidi na kwamba majasusi huinjinia zaidi kuliko vipawa vya siasa, Tatu ni siasa za Chicago ambako nyingi ni za huruma zenye ubaguzi, na nne ni siasa za Arizona ambazo ni za kiliberali.
Kwa Tanzania siasa za Dar es Salama ni moja ya siasa ambazo mtu anaibuka leo na kuwa mwanasiasa mkubwa sana wakuogopwa kisha kesho anazima mpaka kwenye sifuri kabisa na ikimpendeza tunaweka matanga na tanga ndugu. Pole sana Bashiru, dola imeshindwa kukubakiza katika madaraka!
Kwamaneno matatu tu, Utawala wa Mama Suluhu Hasan unaweza kutazamwa kwa pande tatu na zote zikawa na miito tofauti. Kwanza Mama Samia anaweza kuamua kwamba anaongoza miaka mitano hii na hatagombea tena... Yaani kwake inatosha hii mitano kuweka alama kuu Tanzania akapewa heshima yakuitwa Mama wa Taifa kwa legacy atakayoiacha.
Legacy hiyo pamoja na kurudisha umoja wa Kitaifa, itakuwa ya mambo mawili tu muhimu ambayo ni Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, haya yanaweza kuwa legacy kwake mbele ya umma wa Watanzania na akajengewa minara kila pembe ya nchi na kutawazwa kama Mama wa Taifa. Kikwazo kwake ni CCM.
Pili Mama anaweza kuamua kwamba akakubalika ndani ya ccm na hata kuona naweza kuingia kwenye kinyang"anyiro 2025 akiamini dunia bado iko mikononi mwa ccm, Kwanadharia hiyo atalazimika kuendesha nchi kwa mkono uleule tuliko toka. Hapa atakumbana na kikwazo kwake ambacho ni wanamtandao ndani ya ccm na upande wa pili ni umma wa Watanzania ambao kwa namna moja ama nyingi ulishaikataa ccm na mambo yake yote.
Tatu Mama anaweza kuamua kuuthibitishia umma kwamba anaweza kuongoza nchi zaidi ya watu walivyokuwa wakimfikiria hasa wanaccm ambao kwa asili ni wahafidhina wasioamini kuongozwa na Mwanamke. Hapa anaweza kuongoza nchi kwa mkono wa chuma tukajikuta tunamkumbuka Marehemu Magufuli. Athari za chaguo hili la tatu ni yeye kuwa kwenye hatari kwani atarithi maadui na atatengeza maadui mwisho ukawa mgumu kwake 2025 ikiwa lengo ni kurudi tena.
Na Yericko Nyerere