Kwa Ujanja Ujanja huu Simba Mnajiharibia

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Azam alishinda goli moja bila dhidi ya simba ni katika mchezo mzuri wa kuvutia ambapo timu zote mbili kila moja zilionyesha uwezo na thamani halisi ya usajili wao mechi iliotuacha tukizitathhmini timu kiuwezo nakimkakati.

Ikafuata mechi ya yanga na geita yanga alishinda kwa goli la penati,japo goli lile lilizua sintofahamu baada ya refa kutoa penati ili hali mchezaji yule aliunawa nje kidogo ya box.
Yanga akaibuka mshindi.

Nakuja kwenye point
Matokeo ya Mechi ya Azam na Simba na Matokeo ya Yanga na Geita yakamchanganya sana simba,hivyo wakaapizana kuwa mechi yao na mtibwa watashinda kivyovyote vile!baadhi ya washabiki wa simba walisikika kujiapiza hadi siku ya mchezo asubuhi ya jumamosi!

Unajiuliza Simba mnajitambua kweli?kwanini mnapenda sana msaidiwe na juhudi za nje ya uwanja kuliko kucheza mpira?

Jmamosi asubuhi ktk vijiwe kadhaa tuliongea na kutabiri simba kupewa penati au kadi nyekundu,na kweli yakatokea maajabu.!

Simba wanajiharibia sana katika kukwepa kutafuta changamoto zao na badala yake wanajipangia wapate point tatu kwa njia za pembeni.

Tujiulize Mtibwa wangekua kamili na balance ya mchezo ingekua sawa simba angeshinda mchezo?tukumbuke baada ya mchezaji wa kwanza wa mtibwa kupewa kadi mtibwa waliendelea kulisakama lango la simba kana kwamba wametimia.

Wachezaji simba wakawa wakigusana na waxhezaji wa mtibwa physical contact wanajibingirisha wee na kupiga kelele za maumivu ati wameumizwa vibaya!...mbinu zile ni woga mtupu na kushindwa kupambana na changamoto!

Simba chezeni mpira,fanyeni usajili wa kueleweka kama Singida,Azam,Yanga...mtafanikiwa lakini ujanja ujanja huu hamtajenga!mnakwenda makundi hiyo michongo haitowavusha.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
"Tujiulize Mtibwa wangekua kamili na balance ya mchezo ingekua sawa simba angeshinda mchezo?" - Mleta uzi alisikika

Pichani: Mleta uzi alipokutana na mwandishi wetu mwandamizi.

Usisahau kutoa comments na kulike kama umefurahishwa na habari hii, ahsanteni.
 
Kwani huu mchezo uliangalia.peke yako? Mbona unazungza tofauti na mchezo ulivyokuwa? Au ndiyo vile kuwa huko Yanga yamejaa mapooza tupu?
 
Hakika ukiwa gongowazi na mwikombelenyuma ni hamnazo,achana na Simba inayowapiga wageni nje&ndani
 
Kwa io zile kadi nyekundu hazikuwa Halali? Rafu aliyochezewa Sakho?
Na ile ya pili?
 
Utopolotu mtupu.

Kipimo cha timu kijitambua ni kuzipa umuhimu mechi za kimataifa siyo ushindi wa mchongo kwa timu za ndani.

Umetumia akili za pimbi kuandika
 
Hakika aliewaita utopolo aliwaza mbali sana
 
Punguza makasiriko na timu ya wenye akili timamu

SIMBA SC ni timu ya wenye akili timamu.
 
Mleta mada hana hamu na haya mashambulizi kaikacha thread yake
Kwi kwikwi
 
Huu uchambuzi au ushabiki, gori tano zimekuchanganya
Goli moja la Dube lili make sense kuliko magoli matano yaliyokosa ufundi wala hamasa...

Hakuna kitu kitakupa raha ktk mchezo kama game challenge..
Unacheza eleven against 9 halafu unashinda goli tano mnaruka na kushangilia!

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…