Kwa ujinga huu, sitamuamini mtu hasa vijana

balibabambonahi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Posts
15,771
Reaction score
14,294
Kuna huyu kijana alipost anatafuta kazi, nikamtafuta akadai ana nauli pungufu.

Tukakubaliana nimtumie nusu nauli. Nilimtumia lakini siku ya kuja akawa amezima simu na kufuta picha aizonitumia watsaup. Nilikomenti jinsi alvyofanya baadaye akanitafuta akidai alivamiwa na vibaka wakampora kila kitu.

Akaniahidi atakuja, kweli akaja Dar Es Salaam hadi nyumbani, nikamuonesha maeneo ya kazi zangu. Nikawa nafanya naye huduma ya wakala wa miamala ya pesa.

Ikabidi awe anawahi kufungua maana alikuwa anakaa karibu. Asubuhi ya Leo kachukua laki sita, simu mbili na line NNE na ametoa pesa zote kakimbia. Pale getto alipokuwa anakaa vijana wenzake kawaibia nao pesa zao.

Ripoti nimetoa kituo cha polisi Sealander bridge na RB ninayo.
 
Kuna mwingine sijui ni jana au juzi kaleta uzi kuwa member mwenzetu fulani amefariki msiba uko sehemu fulani.
Baadae watu wanatoa pole si moderator wakagundua marehemu na aliyeleta habari ni mtu mmoja ikabidi waunganishe zile I'd πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Sema na wewe unazingua, yani unambeba mtu humu mitandaoni humjui vizuri unaenda kumweka kwenye miamala?
 
Hakika usimwamini mtu usiye mjua
 
Humu kuna majambazi mkuuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜Š
 
😱😱😱 aiseee
 
Chai zimekuwa nyingi tunakimbilia kutoa pole na misaada, kama ni kweli mkuu pole sana mkuu wakati majukwaa yanatumika kutukwamua vijana kiuchumi na kupata fursa za ajira wengine wanazitumia kwa wizi na utapeli wengine wanadiriki kusema mtu fulani kafariki ili wachangiwe kumbe ni ID yake naomba uongozi wa JF kwa ujumla na content controllers mtusaidie hivi vitendo vitakidhiri visiposhughulikiwa, JF itageuka uwanja wa matapeli na wezi
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† watu wabaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…