Kwa ujio huu, Prof JAY ndio baba wa Hiphop Tanzania

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,222
Reaction score
4,689
Profesa Jay amekuja na video mbili kali alizofanya na directors wa kitanzania.

1. kipi sijasikia aliyomshirikisha Diamondplatnumz

Hii video ni kali japo sijaona Adam Juma akifanya jipya kwenye video zake kwa sasa, ila kibongobongo ni video poa.




2. Tatu chafu

Hii ndio video yangu bora katika video alizowai fanya Prof, amefanya na director mgeni kidogo anitwa Hefemi



Hii comment ya Bongofive kwenye Youtube imemaliza kila nilichotaka kusema

 
Last edited by a moderator:
Hii tatu chafu ni kama idea ya stopa tu..
Kweli muziki umevamiwa....bwana mdogo hakuna kipya saana kwenye music idea zinaboreshwa tu...Ni kama niseme iyo style tatu ya Stopa kakopi kwa Jay Moe kwenye Story tatu. Na hii ni kwa dunia nzima.

Jay anafanya Hiphop ya kijanja sana, sio mambo ya kuonyesha usela mavi kama watoto wa Tamaduni music.



Izovideo ndio mambo tunayotaka kuyaona kwa wana Hiphop wa sasa.
 
mr gentleman

ngoma ya stoppa na jay mo ni vitu viwili tofauti!ila prof J kapita alipopita stoppa katika chorus ya style tatu
 
Last edited by a moderator:
mr gentleman

Mkuu Tamaduni Music wanaonyesha usela mavi gani? Mbona wako fresh tu.
 
Last edited by a moderator:
Ok, ngoma iko sawa, lakini mwambie ajitahidi kufanya mazoezi pia, maana obessity ni noma. Juzi tu nilikuwa namwangalia Missy Elliotte, kapunguza body yuko poa sana siku hizi.
 
Mkuu Tamaduni Music wanaonyesha usela mavi gani? Mbona wako fresh tu.

Mi mwenyewe nashangaa maana tamaduni music yenyewe inaundwa na vichwa huru labda angesema Niki Mbishi au Songa n.k anaonyesha usela mavi halaf tumhukumu kila mtu kivyake.
 
Lakin mbona kama hajachangamka...yan kama anajilazmisha vle au ndo heavy weight yenyewe hiyo.
 
Hii tatu chafu ni kama idea ya stopa tu..

Mkuu Somji Juma juma hebu twambie Prof Jay kakopy nini kwenye wimbo wa Stopa?
Neno tatu chafu?
Ideal nzima ya wimbo?
Style ya wimbo?
Mtiririko wa wimbo?
Melody ya wimbo?
Title ya wimbo?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Somji Juma juma hebu twambie Prof Jay kakopy nini kwenye wimbo wa Stopa?
Neno tatu chafu?
Ideal nzima ya wimbo?
Style ya wimbo?
Mtiririko wa wimbo?
Melody ya wimbo?
Title ya wimbo?

Idea
Tone ya chorus
 
Last edited by a moderator:
Kipi sijasikia video kama haiko poa sna hata kwa standards za Adam. Rangi iko poor kwa mtazamo wangu
 
mr gentleman

Af nahisi we ndo umevamia muzik sidhani kama video ni among the five pillars of Hip hop, Tamaduni do hip hop sikiliza Kivyo vyote by One
 
Last edited by a moderator:
mr gentleman

ngoma ya stoppa na jay mo ni vitu viwili tofauti!ila prof J kapita alipopita stoppa katika chorus ya style tatu

Hii tatu chafu ni kama idea ya stopa tu..

Du sijaisikia hio ngoma ya tatu chafu maana nipo minjingu porini nakata mbuga hakuna 3G ni mwendo wa EDGE....Ila style 3 ya stoppa ni track hatari sana ile...."Mi lov a citi weda si don wi mi bway stackin togeda ina concet mi gi dem flavor in dar is hot like ina lilo pot slam a gyal 2times mi jus float" lol
 
Last edited by a moderator:
Mtazamo wangu prof anajitahidi kurudi ila no new ideaz...''Chungu ka Sifongo '' story zile zile za 2001.
Nadhani angewatafuta ndugu zake kina Big Willy na Terry mzee wa Mineli warudi kama HBC wangeweza coz nikiwa kama mpenzi wa Hip Hop ya Bongo wale jamaa walikuwa wanatengeneza Crew hatari sana ila kwa style hii naona bado sana.

Mpaka sasa sijaona Album bora ya Hip Hop kwa Bongo zaidi ya FUNGA KAZI.
 

Old tymer Mwakalinga..

You can say it again bab ....
 

Funga Kazi ilikuwa balaa ilikuwa ina bang sana kuanzia kibo mpaka oldonyo majita walikuwa wanaazima sana ile Tape.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…