Kwa ukiritimba alio nao Dangote bora atafutwe mwekezaji mwingine

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Mwanzoni nilidhani Dangote ni mtu safi ila baada ya kufuatilia nimegundua ni mtu mbinafsi anayependa apate peke yake. Hataki ushindani. Huko kwao Nigeria analaumiwa kushika biashara nzima ya mafuta peke yake kwa kisingizio cha uzalendo. Pia kuna malalamiko kutoka nchi kadhaa za Afrika kuhusu Dangote kujimilikisha biashara ya cement.

Ninashauri Dangote asibembelezwe. Kama hataki atafutwe mwekezaji mwingine asiye na longolongo. Sio sahihi mtu mmoja kufakamia keki ya taifa peke yake. Ni ukiritimba usio na sababu. Kama atajenga hiyo Oil Refinery basi asitake kuzuia watu wengine kufanya biashara ya mafuta au yeye kuwa final say wa hiyo biashara.

Dangote anaihitaji Tanzania kuliko Tanzania inavyomhitaji yeye. Anavyosema anaenda Kenya ni kutaka kutupima. Tanzania ina watu wengi sana na pia ni njia ya kwenda kufanya biashara na DRC, Zambia, Burundi, Malawi na Rwanda. Akiwekeza Tanzania ana uhakika wa kufanya biashara na hizo nchi kuliko akienda Kenya ama Uganda.
 
Dangote ni ***** usinielewe

Nisikie inatosha, wa TZ ni limbukeni wa ufahamu duniani hakuna sababu ya detail
 
Serikali inashindwa vipi kuingia ubia na Dangote kujenga hiko kiwanda?

Itoe mtaji nusu kuchagia ujenzi.

Itapunguza nguvu ya Dangote.
 
Mwanzoni nilidhani Dangote ni mtu safi ila baada ya kufuatilia nimegundua ni mtu mbinafsi anayependa apate peke yake. Hataki ushindani. Huko kwao Nigeria analaumiwa kushika biashara nzima ya mafuta peke yake kwa kisingizio cha uzalendo. Pia kuna malalamiko kutoka nchi kadhaa za Afrika kuhusu Dangote kujimilikisha biashara ya cement.

Ninashauri Dangote asibembelezwe. Kama hataki atafutwe mwekezaji mwingine asiye na longolongo. Sio sahihi mtu mmoja kufakamia keki ya taifa peke yake. Ni ukiritimba usio na sababu. Kama atajenga hiyo Oil Refinery basi asitake kuzuia watu wengine kufanya biashara ya mafuta au yeye kuwa final say wa hiyo biashara.

Dangote anaihitaji Tanzania kuliko Tanzania inavyomhitaji yeye. Anavyosema anaenda Kenya ni kutaka kutupima. Tanzania ina watu wengi sana na pia ni njia ya kwenda kufanya biashara na DRC, Zambia, Burundi, Malawi na Rwanda. Akiwekeza Tanzania ana uhakika wa kufanya biashara na hizo nchi kuliko akienda Kenya ama Uganda.
Kwa taarifa yako serikali inamwogopa tajiri
 
Serikali inashindwa vipi kuingia ubia na Dangote kujenga hiko kiwanda?

Itoe mtaji nusu kuchagia ujenzi.

Itapunguza nguvu ya Dangote.
Terms and conditions must fair Tanzania
 
Back
Top Bottom