tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,491
Naukumbuka sana uongozi uliotukuka wa Leodegar Tenga kama Rais wa TFF na mafanikio mengi aliyoyafanya hasa hasa kwa kuunda kamati mbalimbali ndani ya TFF ambazo zilikuwa na zinafanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu bila kuingiliana na pia kuhakikisha kila kiongozi anawajibika kwa mujibu wa kanuni ndani ya TFF na hata kiwango cha juu kabisa kwa viwango vya FIFA kwa timu ya Taifa
Lakini baada ya uongozi wa Rais Tenga kuondoka madarakani na kuingia Jamal Malinzi tukaanza tena kuona watu wakifanya ofisi kama mali yao binafsi,ajira hazitangazwi tena,ufujaji wa fedha za FIFA kwa maendeleo ya soko nchini,kutokuwa wazi kwa program ya maendeleo ya soko nchini na nk
Baada ya Malinzi kuishia gerezani huku kesi yake ikiwa mahakamani tunashuhudia tena sakata lingine la Wambura na Rais wake Karia kuhusu ubadhirifu wa miaka ya nyuma kwa viongozi wa ilikuwa FAT.
Kiukweli tumekuwa tunachagua viongozi ambao kazi yao ni mizozo tu na kutafuna pesa ya Shirikisho la soko nchini TFF bila kuangalia maendeleo ya mpira na kuwa na malengo kuhusu soka letu.
Wakati nchi zingine wanaweka malengo ya muda mfupi na mrefu kuhusu maendelo ya soko sisi huku tunabaki kutafuta wachawi ndani ya uongozi na kuoneana wivu ndani ya uongozi wa TFF.
TFF watanzania wanataka maendeleo ya soko ni lini tutashiriki mashindano ya bara la Africa au ni lini tutakwenda kombe la dunia hayo ndiyo watanzania wanahitaji na si kujua nani kaiba pesa sijui kagushi barua sisi hayo hayatusaidii kabisa.
Kuna haja ya serikali kuingilia mchakato wa kupata viongozi hapo TFF ili kweli tujue kuna uongozi unaojali maslahi mapana ya soko la Tanzania kuliko ilivyo hivi sasa.