Kwa uongozi huu wa TFF hakuna tena maendeleo soka nchini

tatum

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
5,786
Reaction score
4,491
Naukumbuka sana uongozi uliotukuka wa Leodegar Tenga kama Rais wa TFF na mafanikio mengi aliyoyafanya hasa hasa kwa kuunda kamati mbalimbali ndani ya TFF ambazo zilikuwa na zinafanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu bila kuingiliana na pia kuhakikisha kila kiongozi anawajibika kwa mujibu wa kanuni ndani ya TFF na hata kiwango cha juu kabisa kwa viwango vya FIFA kwa timu ya Taifa

Lakini baada ya uongozi wa Rais Tenga kuondoka madarakani na kuingia Jamal Malinzi tukaanza tena kuona watu wakifanya ofisi kama mali yao binafsi,ajira hazitangazwi tena,ufujaji wa fedha za FIFA kwa maendeleo ya soko nchini,kutokuwa wazi kwa program ya maendeleo ya soko nchini na nk

Baada ya Malinzi kuishia gerezani huku kesi yake ikiwa mahakamani tunashuhudia tena sakata lingine la Wambura na Rais wake Karia kuhusu ubadhirifu wa miaka ya nyuma kwa viongozi wa ilikuwa FAT.

Kiukweli tumekuwa tunachagua viongozi ambao kazi yao ni mizozo tu na kutafuna pesa ya Shirikisho la soko nchini TFF bila kuangalia maendeleo ya mpira na kuwa na malengo kuhusu soka letu.

Wakati nchi zingine wanaweka malengo ya muda mfupi na mrefu kuhusu maendelo ya soko sisi huku tunabaki kutafuta wachawi ndani ya uongozi na kuoneana wivu ndani ya uongozi wa TFF.

TFF watanzania wanataka maendeleo ya soko ni lini tutashiriki mashindano ya bara la Africa au ni lini tutakwenda kombe la dunia hayo ndiyo watanzania wanahitaji na si kujua nani kaiba pesa sijui kagushi barua sisi hayo hayatusaidii kabisa.

Kuna haja ya serikali kuingilia mchakato wa kupata viongozi hapo TFF ili kweli tujue kuna uongozi unaojali maslahi mapana ya soko la Tanzania kuliko ilivyo hivi sasa.
 
Mimi naona kwa uongozi huu wa ccm wakuogopa mpaka katuni za masoud kipanya...mjuwe viwanda vyenu vitapatikana coco beach kweny viloba vyenye watu.
 
Tatizo la wambura na huyu msomali ni kuogopana, msomali anamuogopa sana wambura na ndie kajenga zengwe lote hili ktk kujaribu kumpoteza wambura. badala ya kukaa pamoja kujenga soka letu ameanza kuleta mambo ya kipuuzi kabisa.
 
Mimi naona kwa uongozi huu wa ccm wakuogopa mpaka katuni za masoud kipanya...mjuwe viwanda vyenu vitapatikana coco beach kweny viloba vyenye watu.
Mbona umeamua kuharibu mada ya mwenzio?
 
Watu wote wanaongoza TFF Huwa ni wapigaji tu naona

Ova
 
Akna Malinzi hawakuwa wakijua zaidi mambo ya soka lakini walikuwa na upeo fulani katika management ya michezo hasa kwenye kuifanya kuwa kibiashara zaidi. Ni bahati mbaya sana kuwa wameshitakiwa kwa makosa ya irregularities za pesa na sio wizi wa moja kwa moja, Ngoja tutaona utetezi wao pale kesi za msingi zitakaposikilizwa ili ukweli ujulikane.

Hawa wa sasa heanda zikawa ni porojo zilezile za siku zote za kujiita 'watu wa mpira' huku zikichagizwa na sijui 'watu wa system'. Suala la Wambura linawafumbua macho waliokuwa usingizini japo wengine waliyajua haya tangu awali.

Ni muda tu utatupa ukweli wa mambo haya na majuto ni kukuta tumepoteza muda wa kupata japo mwelekeo wa kufanya mambo yetu.
 
Rais wa TFF ni Msomali.
Makamu aliyesimamishwa hafai kwa lolote. Tapeli mzoefu.
Wanataka kuajiriwa Katibu Mkuu Mrundi.
Nani katuroga?
 
Kwenye vyama vya soka na michezo kuna umafia wa hali ya juu: Fifa ya Havalange na Blatta, CAF ya Issa Hayatou TOC ya Samaranch nk. Hata huyu Infantino lazima a-deal na wapinzani wake kikamilifu.

Vv
 
Mimi naona kwa uongozi huu wa ccm wakuogopa mpaka katuni za masoud kipanya...mjuwe viwanda vyenu vitapatikana coco beach kweny viloba vyenye watu.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] uongozi unaoshindana Na Mange kimambi kila siku
 
We nae ndio bure kweli, yani eti nakumbuka TFF ya tenga kwa kuunda kamati me nilizani alifikisha timu ya taifa sehemu flani ambapo wenzie wameshidwa
 
Wote wapigaji tu..natamani kweli Wambura aendelee kufunguka tujue mengi
 
Unamuhukumu mtu wakati:
1. Siku ya kutoa hukumu yy hayupo
2.Mashaidi muhimu hawapo.
3.TFF wanahakiki document ,utazani wao ni TAKUKURU wakati utaalamu huo hawana.
4.Kampuni ambayo nyaraka zake zimefojiwa hawajahojiwa.
Alafu TFF mnajifanya mmefanya maamuzi,hayo maamuzi yenu TFF hayana tofauti na maamuzi ya vikao vya walevi.
 
Alikataa kuhudhuria kwenye kikao kaitwa mara kadhaa ila kwa ujeuri na utaita au umwamba hakuenda
TFF hamna sehem waliosema jamaa aliitwa ,wenyewe waliamua kitisha kikao basi.
 
Alikataa kuhudhuria kwenye kikao kaitwa mara kadhaa ila kwa ujeuri na utaita au umwamba hakuenda

acha uongo mtoto wa kiume utavalishwa sketi Wambura kapewa barua jnne jtano kamati inakaa ,katuma wakili wakamkata wakasema tayari maamuzi yashatoka juu sasa wewe ulitaka afanyaje
 
Back
Top Bottom