KWA UOZO ULIOPO NECTA; Ponda aliona mbali kuanzisha movement ya kumn'goa Ndalichako

kigu

Senior Member
Joined
May 27, 2012
Posts
183
Reaction score
74
akihutubia maelfu ya waislamu katika viwanja vya kidongo chekundu jijini dar es salam,katika kuhitimisha maandamano ya kupinga filamu ya kumkashifu mtume, shekh Ponda aliuwambia umma wa waislamu waliokuwa wakimsikiliza kwa makini wajiendae kwa maandamano makubwa na ya kisayansi ya kwenda kumg'oa Ndalichako NECTA ,kwa kuwa ameshindwa kazi .........na watu wote walio kuwepo uwanjani hapo, walimuunga mkono kwa kunyoosha mikono juu.





TUKIWEKA UDINI KANDO........KWA HILI SHEKH PONDA ALIONA MBALI!!!, WALAU AUNGWE MKONO KWA HILI.



 
...
TUKIWEKA UDINI KANDO........KWA HILI SHEKH PONDA ALIONA MBALI!!!, WALAU AUNGWE MKONO KWA HILI.
Hatuwezi kumuunga mkono mahabusu. Kama ni mtu wa kung'olewa, basi ni Shukuru Kawambwa!
 
Wewe mwenyewe ondoa Udini kwanza...mana hapo Kidongo Chekundu mlikuwa nyie Waislamu...
 
ni ujinga kumlaumu dr ndalichako kwanini watoto wamefeli mitiani mana yeye pamoja na watuwake wa baraza ndyo wamesabisha wanafunzi wafeli, kazi kubwa ya baraza ni kutunga mitihani na kusahisha mitihani, wao hawashuliki na kufundisha wanafunzi au kuandaa walimu wanaofundisha wanafuzi, matokeo mabovu yanatokana na sera mbovu katika mfumo wa elimu. so hayo yanayotokea baraza nimatatizo ya kawaida but cyo sababu ya wanafunzi kufeli!
 
Shida ya kuandikia thread kwenye nyumba ya mazoezi ya jnsi ya kutumia jambia, kujifunzia Judo na karate
 
Sasa hapa inamaana ndalichako amesahihisha vibaya! Hueleweki au labda huelewi system! Huyo mama hasahihishi!
 
Mleta mada namshangaa sana, yani watoto hawasomi kazi ngono, face book na kujifanya wanakwenda na wakati, wanashindwa mtihani,halafu Mkurugenzi aondolewe?Uozo wa Ndalichako ni upi?Hii nayo kali
 
NECTA wameshindwa kuweka database la ku sort shule online.

Nilikuwa nataka kuanza kuandaa Gap Analysis kati ya shule kumi bora na shule kumi zilizofanya vibaya kabisa, kulinganisha kuanzia uongozi, jiographia, resources etc kwa kadiri inavyowezekana.

Lakini sina hata pa kuanzia.

Data zipo, hili suala si natural disaster tuseme kwamba hawakujua matokeo yanakuja (hata natural disaster watu wanajiandaa)

Sasa hivi nikitaka kulinganisha shule kumi bora na kumi zilizofanya vibaya kabisa siwezi.

Kuna watu wana mi system inahitaji data tu kufanya analytics, hawana data.

Sie tuna mi data kibao imekaa tu, hatujui kui connect.

Hata ki website chenye simple database tu hatuwezi.

Aibu!
 
Hata kama serikali inalaumiwa kwa haya matokeo laa pia ni changamoto kubwa sana kwa WAZAZI kuhusu malezi ya watoto..
 
Mkuu aya za dini yenu zinawazuia kujenga shule na kuziendesha mnavyo jua ninyi?
Au aa hizo ni za kuwaeleza ufundi wa kuandamana tu!
 
Angalia vitu vya kupost unaweza kumuunga mkono hadi taahira
 
Utamng'oa Ndalichako, utamuondoa Waziri Kawambwa, lkn next year ndio watafeli maradufu.
Hii trend ya kufeli itaendelea towards the worst hadi watakapoibuka watu majasiri wa aina ya Mahamoud Mringo kuja kung'oa system nzima, ikiwa ni pamoja na kuthamini taaluma ya ualimu.
 
Mahmoud Mringo ni nani mkuu?
Hebu tupe cv yake!
 
Hao wenzetu ndo upeuo wao ulivyo! Utashangaa hapo aliyepost thread hii ni msomi mzuri tu lakini karoho kale kalusferi kanawasumbua. Ndalichako ndo anawalipa mishahara walimu, anayenunua vifaa vya kufundishia na kujifunzia?
 
bunge huwa linarushwa live, au huwa haufauatilii?............ uozo wa ndalichako,kamuulze mbatia atakuelewesha vizur!!
 
acha ujinga wewe.nadhani wewe ni miongoni mwa waliofeli au kama si wewe mwanao au ndugu yako. Ndalichako ajiuzulu kwa wanafunzi kujibu ujinga kenye mitihani ,ulitaka awape max wakati wanachora mazombe yanavuta bangi?wewe ni mtu wa namna gani?NDALICHAKO ANASTAHILI TUZO YA UTUMISHI ULIOTUKUKA. kumbika kabla hajaingia hapo NECTA watu walikuwa wanauza mitihani kama nyugu na mapepa yalikuwa yanazagaa mitaani hadi akina mama wanauzia vitumbua.Alifanikiwa kwakiasi kikubwa kuondoa na kusambaratisha mtandao wa watumishi hao hapo necta.na kwa sababu walikwishakuwa vingunge hapo walianza kumtafutia kashfa na hujuma mbalimbali lakini dactari huyu wa philosofia wa ukweli hajatetereka hadi leo.wewe huyajui hayo? au umezaliwa jana? wewe nikikuuliza ajiuzulu kwa lipi utajibu nini?yeye ni chombo huru cha kutunga na kusahihisha mitihani kwa mujibu wa silabasi.ninakushauri ukitaka ufaulu au ndugu yako afaulo ahesihimu shule na jiepushe na starehe.shule ina nidhamu yake shule zinazozingatia nidhamu na maadili ndio zilizofaulisha.Hapa simaanishi seminari za kikristo tuu hasha hata zile za kiislamu KAMA NYASAKA ISLAMIC YA MWANZA nimeiona matokeo yake ni mazuri kabisa. sasa wewe unasoma sekondari na mzazi wako anakununulia simu eti anakupenda badala ya kusoma unachati usiku mzima kwenye facebook na kuchangia mada jamii forum utafaulu?Tuache siasa kwenye mabo ya msingi BIG UP MAMA NDALICHAKO
 
hebu soma hii toka Tanzania Daima ndo utaja Necta hawapo makini

WAKATI mjadala wa matokeo mabaya ya kidato cha nne ukiendelea kulitikisa taifa, kashfa mpya ya matokeo hayo imeibuliwa.
Kashfa hiyo mpya imeibuliwa na Mkurugenzi wa Shule ya Green Acres, Julian Bujugo, kwamba matokeo ya baadhi ya shule nchini ikiwamo yake yamechakachuliwa.
Akizungumza na gazeti hili jana, Bujugoalisema kuwa baadhi ya wanafunzi kwenye shule yake hawakufanya mitihani ya kidato cha nne, lakini matokeo yanaonesha wamefaulu kwa kupata alama za juu.
Alitaja mfano wa mwanafunzi, Humphrey Sanga, mwenye namba 01197/148, ambaye hakufanya mitihani hiyo lakini matokeo yanaonesha amefaulu kwa kupata alama nzuri.
"Huyu mwanafunzi tulimsimamisha na hakufanya mitihani, lakini matokeo yake yanaonekana amepata hivi; Civics D, Historia D, Jiografia C, Kiswahili D, English C, Physics D, Chemistry C, BiologyC, Basic Mathematics D, ambapo amepata daraja la tatu pointi 24," alisema Bujugo.
Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya ‘Arts'.
Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alamaza masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa.
Alimtaja mwanafunzi mwingine aliyefanya mtihani huo lakini matokeo yake yanaonesha amewekewa ‘absent' na mwanafunzi mwingine, Mbazi Volta, hakufanya mitihani lakini amepewa alama za ufaulu.
"Matokeo hayo yananipa wasiwasi kwamba yanaweza kuwa yamechakachuliwa," alisema Bujugo.
Mkurugenzi huyo anaiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kurudia kusahihisha mitihani hiyo ili kuondoa ukungu ulioligubika taifa kwa sasa kuhusu matokeo ya kidato cha nne.
"Naomba usahihishaji urudiwe, maana huu ni ubabaishaji mkubwa…matokeo hayo yamewaathiri watoto kisaikolojia na sijui watakwenda wapi?," alihoji.
Alisisitiza kuwa usahihishaji urudiwe kwani katika shule hiyo wanafunzi wenye uwezo mkubwa tangu walipoanza kidato cha kwanza ndio waliofanya vibaya wakati waliokuwa wakifanya vibaya, wameibuka na alamaza juu.
Mkurugenzi huyo alisema wazazi wa watoto hao wanatarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki hii kujadiliana kuhusu matokeo hayo na hatua za kuchukua.
Akitolea ufafanuzi suala hilo, Msemaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), John Nchimbi, alisema si kweli kuwa matokeo hayo yamechakachuliwa bali ni matokeo halisi ya shule hiyo.
Alisema iwapo mkurugenzi wa shule hiyo ana shaka na matokeo hayo, alitakiwa kufika katika ofisi za baraza hilo ili apatiwe taarifa sahihi kabla ya kutoa taarifa katika vyombo vya habari.
"Mi nimeangalia hayo majina, naona yapo sawa na hata huyo mwanafunzi ambaye anasemekana hakufanya mitihani na akapewa alama…napenda kusema kuwa alama alizopewa si zake na hata katika orodha yetu anaonekana kuwa hakufanya mitihani," alisema.
Katika hatua nyingine, Waziri wa wizarahiyo, Dk. Shukuru Kawambwa na wenzake, wamekuwa bubu kueleza endapo wako tayari kujiuzulu au la.
Tanzania Daima ilifika wizarani hapo jana kutaka kuonana na Waziri Kawambwa ili atoe msimamo wake, mwandishi alijibiwa kuwa waziri huyo alikuwa kikaoni na asingeweza kutoka.
Hata waziri alipopigiwa simu pamoja nakutumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakupokea wala kujibu ujumbe huo.
Kwa upande wake, katibu mkuu wa wizara hiyo naye hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa alikuwa kikaoni.
Naye Naibu Waziri, Philipo Mulugo, alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi kueleza msimamo wake, simu yake iliita bila kupokewa na hata hakuwa tayari kujibu meseji ya ujumbe mfupi.
 
Mpaka pale walimu watakapo thaminiwa na kupewa haki zao za msingi kama teaching allowance, nyumba, mshahara toshelevu nk ndio hii hali itapungua kama si kuondoka kabisa. Otherwise tutaendelea na ma zero kila mwaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…