Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Moja ya sifa ya kuna demekrasia ni uwepo wa utawala bora, dhana hii ya utawala bora imekuwa na mtazamo tofauti tofauti kutoka kwa mtu mmoja kwend akwa mwingine, kila mtu amekuwa akiweka kipimo cha kumjua mtawala bora kulingana na na jinsi alivyokuwa akitegemea kuongozwa na mtawala au kiongozi.
Wapo wanaosema kiongozi au mtawala bora ni mwenye kaliba ya upole wengine ukali, wengine anaechukua hatua papo kwa papo wengine anaeachia mchakato ulioratibiwa wa namna ya kuchukua hatua dhidi ya jambo fulani, wapo wanaotaka anayefanya miradi wengine anaewafanya watu waone unafuu wa maisha, ilimradi kila mtu ana mtazamo wake.
Ukiachilia mbali sifa za jumla za kiongozi au mtawala aliye bora kama anatakiwa kuwa muwajibikaji, muwazi na anayezingatia mamlaka ya katiba kwako sifa zipi ukiziona unasema hakika huyu ni kiongozi au mtawala bora, au ungetamani kumpata kiongozi mwenye sifa zipi ili uone umepata mtawala aliye bora?