Kwa UTAMADUNI WENU: Je wajua nini kinasababisha Jino kuoza na Kutoboka?

Kwa UTAMADUNI WENU: Je wajua nini kinasababisha Jino kuoza na Kutoboka?

COARTEM

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2013
Posts
3,603
Reaction score
3,658
MODDS nawaomba msihamishe hii post kwa FAIDA yetu sote:
Watu wengi Tanzania wanakuwa Vibogoyo au nusu vibogoyo kwa kupoteza meno yao kwa kuyang'oa kutokana na maumivu makali waliyoyapata.
SWALI: Kwa ufahamu wako mwana JF na hasa kwa Ukiangalia Utamaduni wa nyumbani kwenu...Je nini kinasababisha jino kuoza na kutoboka? Je wewe unafahamu matibabu ya jino linalouma?
STORY ZA KIJIWENI:
1. Jino linatobolewa na Mdudu..anatoka jino moja na kuhamia jino lingine tena unamsikia kabisa anavyotembea.
2. Dawa ya jino ni Kung'oa
3. Matatizo ya kuoza meno ni ya kurithi.

Naombe tupate General views ya wana JF kabla ya kuwaleta wataalamu husika kutupa elimu.
 
dawa yake ni mzizi wa mlonge ukitumia huwez kupata tena tatizo la meno
 
Mimi naijua dawa ya jino, hayo ya stori za vijiweni ni kwasababu hawajapata tiba.
Pia jitahidi kusafisha kinywa chako mara kwa mara usiruhusu mabaki ya chakula kinywani make ndio chanzo cha ugonjwa.
Mkuu tusaidie mkuu hio yada maana waathirika ni wengi sana aiseee.

Kama una muda tuhabarishe na sisi aiseee
 
Mkuu hio ya mzizi wa mlonge unachemsha au unafanyaje??

Na hiyo ni kwa jino lililotoboka au jino la kulegea tu??
hiyo unatafuna kwa kutumia upande usio na tatizo then yale mate una yahamishia upande wenye matatizo unaacha kwa robo saa alafu unasafisha mdomo usimeze, hiyo ni kwa matatizo yote ya meno
 
hiyo unatafuna kwa kutumia upande usio na tatizo then yale mate una yahamishia upande wenye matatizo unaacha kwa robo saa alafu unasafisha mdomo usimeze, hiyo ni kwa matatizo yote ya meno
Unaitumia kwa muda gani mkuu??

Au mara nyingi mpaka tatizo uone tatizo limepotea kabisa??
 
meno kutoboka n kwasababu ya bacteria wanao vunja vunja mabaki Ya chakula(sukari) na kutengeneza acid......HIYO ACID NDO HUABAABISHA MENO KUOZA ......dawa ya haya magonjwa n kuhakikisha usafi wa kinywa mda wote kwa kuswaki kila baada ya kula.....
 
Back
Top Bottom