Kwa utendaji huu ukimlinganisha na Hayati Magufuli, ni busara Rais Samia asigombee 2025

Pamoja na mapungufu yake, JPM alikuwa ana uwezo wa kumiliki maamuzi yake katika kila jambo. Hili lilimfanya ajiamini na kusimamia mawazo/maamuzi yake hata kama yalipingwa na ulimwengu mzima.

Sasa kwa mama yetu ni kama vile haamini bado kuwa yeye ndie raisi, ni kama vile hajui nguvu aliyokuwa nayo na mbaya zaidi ni wazi kaweka bayana kwa washauri wake kuwa hana dira. Hili linawapa nguvu wasaidizi wake kufanya maamuzi bila kumshirikisha ipaswavyo ama kupindisha uhalisia hasa wa athari ya maamuzi hayo. Hii inamgharimu mama pale athari inapakuwa hasi, inabidi kutoa kauli kutuliza jazba ambapo in reality linafikirisha juu ya alikuwa wapi mambo yakiamuliwa.

Japo kuna baadhi ya watu watapinga kwa vile wamampenda mama, ila ni wazi mama hajui anakokwenda, hana dira na hana kauli katika maamuzi yake.

Na bahati mbaya yake zaidi ni kitendo cha kutanguliwa na mtu kama Magufuli ambae alama yake hata kama si nzuri ilikuwa ni kubwa. Kwa sasa mama kila akifanyacho anamithilishwa na Mafuguli kwa mizani ya kuwa yeye ni dhaifu, kiasi uwepo wake hauna tofauti yeyote na kutokuwepo kwake. Rejea vikauli kadhaa vya maelekezo alivyovitoa ambavyo vilipuuzwa tu.
 
Huyu Bibi Tozo tuliyenaye sasa anatupeleka siko!
 
Umemaliza kila kitu,,,,Jambo la Mbowe limemtia Sana Doa,,,
 
Kweli mkuu,ukiondoa tozo mpya na kukamatwa kwa Mbowe,Samia kuna mazuri kafanya kwa huu muda mfupi.
Na ni mambo ambayo yanazungumzika na yanaweza kumalizwa na pande zote zikafurahi, ni suala la muda tu
 
Samahani mkuu naomba niulizie hivi una mtoto ambaye unamsomesha shule za manispaa.
 
Jambo la kwanza JPM hayupo duniani hivyo kubaki kumlilia na kumtaja mara angetuacha wapi au vile haisaidii.Pia usisahau kua wakati wa JPM mawaziri na viongozi waligezwa badala ya kuwatumika watu walimtumikia yeye ndio maana hata kama mtu angefanya madudu vipi lakini kosa lilikua ni kutomsifu na kumtaja taja yeye.Pili watu walimheshimu JPM na sio serikali ndio matokeo tunayoyaona leo.Kwa upande wangu naona nchi inakwenda vyema kama watumishi wanalipwa mishahara,biashara zinaendelea,miradi inaendelea huwezi kusema nchi imesimama au imekosa direction.Najua zipo changamoto zimeletwa na bwana Mwigulu juu ya Tozo na Kodi ya Mapato lakini hizo hazifanyi toconclude kuwa mambo hayaendi.Well inaweza kua ile amsha amsha imepungua kwa mawzili ukiondoa Jafo,yule waziri wa maji,wa afya na wa Tamisemi amabao tunawasikia,walio wengi ni kizazi cha JPM bado wanaomboleza.Hivyo basi tunahitaji kupambana na changamoto kwa kutembea sio kusimama na kulia lia.
 
Mwenyekiti wa CCM hawezi kustaafu mpaka amalize vipindi viwili. CCM haina ubavu wa kumgusa mwenyekiti. Hata tume ya uchaguzi, polisi, majeshi, nk, watasimama na mwenyekiti wa CCM hivyo hivyo hata akiwa boga.
Dua ziendelee tu
 

 
Mkuu mimi naona ikifika wakati wa mtu kuongea ukweli mchungu pasipo kujali kuwa watu watatoka povu la kumfa mtu ama la, itakupasa tu kufanya hivyo. Chanzo kizuri cha mapato ni kile kisichokuwa na ubaguzi wa aina yoyote kwa makundi ya watu na tena kinachoatozwa katika chanzo kimoja kinachofanana cha mapato. Na hii ndiyo hasa sifa ya kipekee iliyopo katika tozo za vifirushi vya simu na kufanya miamala kwa njia ya simu.

Tukianza kuangalia njia katili na zakiubaguzi za hayati JPM za ukusanyaji wa mapato hazikuwagusa na kuwaathiri sana wale walioitwa wanyonge, kwa kuwa biashara zao hazikusajiriwa na kuwa nje ya macho ya mfumo rasmi wa kodi.

Kwa kadiri wafanyabiashara waliokuwa katika sekta iliyokuwa rasmi walivyoshughulikiwa kupitia mkono wa chuma wa serikali kwa maelekezo kwenda TRA, wale waliokuwa katika sekta isiyokuwa rasmi waliona ni jambo jema kufanywa na mtetezi wa wanyonge. Maduka yalifungwa, akaunti za watu zilitolewa fedha kwa maelekezo maalumu, "task force" ikaundwa na kuwa wakala wa kufanya dhuluma, watu walitishiwa, kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi na hata wegine hata kushughulikiwa kwa njia tofauti,.

Lakini yote hayo yakifanyika, jambo hili lilikuwa ni faraja kwa wanyonge kwa walioaminishwa wapiga dili ambao wanashughulikiwa wameliibia taifa letu tajiri kwa muda mrefu. Watumishi wa umma waliponyimwa stahiki zao na wastaafu walipocheleweshewa malipo pesheni zao wanyonge walifurahia jambo hilo kwa kuwa walitamani maendeleo ya vitu kupitia udhalimu uliofanywa na serikali yao pendwa ya wanyonge.

Sasa majira yamebadilika, kapu la hazina ya taifa ni dhahiri linaonekana halina njuruku za kutosha. Chanzo kipya cha kodi cha kizalendo kimeonekana, na tena kina wagusa hata wanyonge, sasa imebakia malalamiko kila kona. Kwa vigezo vyote hiki ni chanzo kizuri mno cha mapato kwa kuwa hakina ubaguzi ila pengine ningeshauri kingepitiwa upya ili kupunguza malalamiko. Nimalizie kwa kufanya marekebisho hayo pia ningeshauri watu wote wenye "taxable income" ikiwemo viongozi wetu walipe kodi.

Ni aibu ya kutafuta vyanzo vipya vya kodi kupitia kuwabebesha watu maskini na fukara wa nchi hii, na kuwapa msamaha wa kodi watu wenye vipato na malupulupu makubwa. Paying taxes is civil obligation.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ