McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Wizara ya Maendeleo ya Vijana, imeanika wazi mwongozo kwa vijana namna ya kuomba na kunufaika na mikopo ya Sh200 bilioni ambayo imekuwa ikitangazwa na Serikali kuwa lengo lake ni kuwawezesha kiuchumi.
Katika mwongozo huo uliotolewa leo Jumamosi Machi 21, 2026, serikali imeeleza kuwa waombaji ni mtu mmoja au kikundi na wanatakiwa kuwa na andiko la mradi au biashara, akaunti ya benki au namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mwombaji au kikundi hicho, pamoja na kuwasilisha barua rasmi ya maombi ikieleza aina ya mradi, kiasi cha mkopo na eneo la utekelezaji.
Aidha, nyaraka muhimu zimetajwa kuwa ni pamoja na kitambulisho cha Taifa (NIDA) au cha mpiga kura, TIN, leseni ya biashara kwa wanaoendesha shughuli tayari, barua ya utambulisho kutoka serikali za mitaa na picha mbili za mwombaji, huku maombi yote yakitakiwa kuwasilishwa kabla ya Aprili 3, 2026 kupitia barua pepe maalum ya [email protected].
Source: Wizara ya Vijana