Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Anaandika, Robert Heriel
Mastermind.
Ufikapo mwisho wa andiko hili utakuwa Umepata haya:
1. Utakuwa umejifunza akili, hulka na silika ya mwanadamu.
2. Utakuwa na uwezo wa kujitambua na kujifahamu.
3. Utakuwa na uwezo wa kuchangamana na watu na jamii Kwa ujumla (kusosholoizi)
4. Itakusaidia kuepuka migogoro na kuwa mtatuzi wa migogoro ndani ya jamii.
5. Itakurahisishia katika shughuli zako hasa zinazohusu kukutana na watu kama vile Biashara, Siasa, sheria, Dini, Sanaa n.k.
6. Itakusaidia kujenga na Kuboresha Ndoa na Familia yako.
7. Itakusaidia kuunda kanuni, sheria, na utaratibu utakaokusaidia katika Mzunguko wako.
Kuna Saikolojia na Sosholojia. Sio maneno mageni Kwa wengi wetu. Zote ni taaluma kubwa zinazojitegemea ingawaje zinaingiliana Kwa kiwango kikubwa.
Sisi wengine tulizaliwa tukiwa na vipaji vya kuwafahamu watu, naam kufahamu Akili, tabia na silika za Watu pasipo hata kusomea. Hii imetusaidia kuyaendesha Maisha Kwa furaha na kuweza kukabiliana na changamoto Kwa urahisi katika mizunguko yetu.
Ukishakuwa mwanasaikolojia na mwanasosholojia ni ngumu kuwa na Adui.
Kila mtoto anapozaliwa, huzaliwa na Akili yaani ule uwezo wa mtu kufikiri, kufahamu, kukumbuka, kuchambua, kuchanganua, kutatua mambo au kuyaweka mambo vile atakavyo.
Akili hutofautiana baina ya mtu na mtu. Kama vile Watu watofautianavyo kimaumbile ndivyo hivyohivyo hata kwenye Akili, wapo Watu wenye Akili nyingi au tuseme kubwa, lakini pia wapo wenye Akili chache au ndogo, labda tuite Upeo mdogo.
Mtoto akizaliwa huja na Akili yake, lakini hukutana na mazingira Mapya na watu wapya wenye Akili huenda tofauti na Ile yake aliyozaliwa nayo.
Ule mchakato wa mtoto kujifunza na ku-adapt mazingira ndio huzalisha kitu kinachoitwa HULKA yaani Tabia.
Hii ni kusema mtoto hazaliwi na Hulka au tabia isipokuwa anazikuta huku Duniani.
Kama Taikon nikiambiwa nieleze Hulka ni nini, basi nitasema ni zile Tabia au Sifa ambazo MTU anaziiga, ana-adapt Kutoka katika mazingira yanayomzunguka, labda ni nyumbani, shuleni, Kanisani au msikitini, au kazini n.k.
Lakini Taikon, mbona tumesikia kuwa kuna Tabia MTU anazaliwa nazo?
Ooh! Bila Shaka Unazungumzia kitu kiitwacho "SILIKA". Ipo tofauti kubwa baina ya SILIKA na HULKA ingawaje zote huwekwa katika kapu moja la TABIA.
~ Silika sio Tabia isipokuwa ni Sifa.
~ Silika ni Sifa ya kimaumbile ambayo mtu huzaliwa nayo. Ni kama vile Akili,
~ Silika hurithiwa Wakati tabia au hulka hairithiwi, bali unajifunza.
Jambo moja la kuweka Akilini ni kuwa SILIKA ni Sifa ya ndani ya MTU/binadamu ambayo hujidhirisha kupitia Hulka au Tabia.
Nimekuchanganya enhee! Subiri, Taikon atakueleza Kwa Lugha nyepesi utaelewa.
Nakupa Mfano, Sifa ambazo mtu huzaliwa nazo ambazo hajifunzi.
I) Ni silika ya binadamu kuzaliwa na Ubinafsi.
Ubinafsi sio Tabia bali ni Silika ya kila Mwanadamu. Kila binadamu ni mbinafsi. Ingawaje kiwango cha ubinafsi kinatofautiana kama ilivyo maumbile mengine
ii) Wivu, Ni Silika ya binadamu kuwa na Wivu.
Hakuna Mwanadamu asiye na Wivu. Ingawaje viwango vinatofautiana.
iii) Tamaa. Ni Silika ya binadamu kuwa na tamaa. Hakuna Mwanadamu asiye na tamaa.
iv) Uvivu. Ni Silika ya Mwanadamu kuwa mvivu. Hakuna Mwanadamu asiye mvivu.
Silika zingine ni kama Hasira, kupenda, chuki, n.k.
Elewa kuwa Mambo mengi tunayoyafanya Duniani yanakinzana na Silika zetu ndio maana tunaona kazi na tabu kuyafanikisha.
Nakupa mfano, Ni Silika ya kila binadamu kuwa Mvivu, sio ajabu inahitaji jitihada kumfanya MTU afanye kazi yaani mpaka itumike nguvu ya ziada, kumlazimisha au kumsimamia MTU ndipo afanye kazi.
Silika ya uvivu huzalisha Tabia ya Uzembe, kupenda shortcuts, n.k. uvivu pia ni chanzo kikuu cha Umaskini,
Upo uvivu wa kufikiri, uvivu wa kutenda na kufanya MTU kutokuchukua hatua.
Silika ya Tamaa huzalisha Tabia ya udokozi, wizi, ujambazi, uzinzi, umalaya, n.k.
Silika ya ubinafsi huchochea Tabia ya Uchoyo, Dhulma, wizi, ufisadi, Uchu wa madaraka n.k. Silika ya Wivu huchochea Tabia ya Uchawi, uuaji, husda, fitna n.k.
Watu wenye maarifa na Werevu hutunga sheria kulingana na silika za binadamu na sio kulingana na Tabia au hulka ya binadamu.
Sheria za Asili zililenga kudhibiti Silika za Mwanadamu ambazo mtu huzaliwa nazo. Na hapa ninapozungumzia kudhibiti ninaelezea kudhibiti kuzidi kuletako maafa Kwa silika hizo.
Maelezo hayo Kwa ufupi ni muhtasari wa SAIKOLOJIA. Ambalo ni somo Pana linalohusu Akili na tabia ya Mwanadamu.
Tunafahamu Mwanadamu anasilika ya ubinafsi yaani anatamani kila kitu kizuri au vitu Bora viwe vyake. Na endapo ukiwa na vitu Bora basi elewa kuwa SILIKA ya binadamu Kwa vile niyawivu basi hawatafurahishwa na Jambo Hilo.
Kueleza mazuri au Mafanikio yako Mbele za Watu ni kujaribu kuchochea silika yake ya Wivu dhidi yako na kulazimisha Tabia ya kijicho, husda na Fitna Kutoka Kwa Watu wanaokuzunguka.
Elewa kuwa hakuna atakayefurahia Mafanikio yako labda awe Mzazi wako(tena awe ananufaika nayo, lakini kama hanufaiki nayo pia hatayapenda), mkeo(halikadhalika naye) na watoto. Hawa ndio angalau Kwa mbali wanaweza kufurahishwa na Mafanikio yako.
Namna Bora ya kuingiliana na kuchangamana na watu ni kujiweka katika Low Key ili kuepusha Misukosuko isiyo na ulazima. Ndio maana unaambiwa usitangaze wala usipende kujionyesha.
Hiyo inaitwa Sosholojia (Sociology), yaani somo linalohusu jinsi MTU anavyohusiana na MTU au jamii inayomzunguka.
Kisaikolojia, unapochangamana na MTU, endapo nguvu kubwa itatumika Sana katika Jambo lolote, elewa kuwa hapo kuna ukosefu Wa moja ya mambo haya mawili au yote Kwa pamoja, nayo ni; AKILI au UPENDO.
Iwe ni kwenye biashara, Dini, Siasa, mahusiano ya ndoa na familia, basi ukiona nguvu kubwa inatumika basi elewa kuwa hapo kunakosekana aidha AKILI au UPENDO au vyote Kwa pamoja.
Upendo ukiwa mwingi, Nguvu inakuwa ndogo. Kinyume chake ni kweli. Akili ikiwa nyingi, Nguvu inakuwa kidogo. Kinyume chake ni kweli.
Kama nilivyowaambia, Taikon nimejaliwa kipaji cha kuelewa SAIKOLOJIA na Sosholojia. Hata katika mahusiano yoyote Yale, mfano ndani ya Ndoa au uchumba.
Ukiona mwanaume unatumia nguvu nyingi kwenye mahusiano yako ujue hapo haupendwi au hauna Akili ya kutosha kuyaendesha hayo mahusiano.
Ukiona unatumia nguvu ya Pesa ili kufanya mahusiano yaende basi ni wazi hapo hakuna Upendo. Au ukiona unatumia nguvu kubwa kumfanya Mkeo au Watoto wakuheshimu basi jua aidha unaakili ndogo Sana au Upendo mdogo Sana.
Mfano unampiga Mkeo kila mara ati kama sehemu ya kumfanya akuheshimu😀😀, jua kuna sehemu unakosea.
Kupiga MTU mzima mwenye Akili hakuleti heshima, isipokuwa kunaleta hofu na woga. Na hofu na woga unazalisha unafiki, kisha unafiki unazalisha mapinduzi.
Muuda wa Sosholojia huchangiwa kwa kiasi kikubwa na Saikolojia za Watu. Akili na tabia za Watu ndio huunda Sosholojia.
Watu wenye Tabia na Akili zinazofanana huunda Sosholojia Yao. Sio ajabu hapo mtaani kuna mitaa ya Watu wa Aina Fulani na mitaa ya Watu wa aina Fulani.
Hiyo haipo tuu katika Maisha ya binadamu Bali Ipo pia katika Maumbile ya dunia(Geomorphology) pamoja na Tabia za Nchi( Climatology).
Maumbile ya dunia yanayofanana labda tutoe mfano katika Maumbile ya miamba, Miamba inayofanana (homogeneous rock) hukaa pamoja au Kwa kufuatana kama mkanda WA dhahabu au almas.
Hata hivyo Ipo Miamba ambayo ni Heterogeneous Rock ambayo hutokana na Miamba mchanganyiko.
Kitabia na Kiakili(Saikolojia) haipendekezwi Watu wenye Saikolojia tofauti kuishi pamoja. Watu werevu na watu wa Daraja la juu, uzuri wa maumbile sio kigezo kikuu cha kuwafanya wakukaribishe kwenye Ukoo na familia Yao.
Ni kweli Kabisa Hulka au tabia zinaweza Kubadilika kulingana na mazingira, lakini weka akilini Hii, Silika ya MTU haibadiliki na haibadolishwi hata iweje.
Zile Sifa mtu alizozaliwa nazo zinabaki kama zilivyo, ni Sifa za Asili. Hata uende hospitalini au Kwa wanasaikolojia hawawezi kubadilisha asili/silika ya MTU.
Katika biashara, biashara inahitaji ubunifu Kwa sababu silika ya binadamu ni kukinai vitu au mambo. Kama utafanya biashara pasipo kuiwekea ubunifu WA hapa na pale kuibadilisha iwe tofauti ya Leo na Jana ni wazi, biashara itakushinda.
Ndio hata siku hazifanani ili kuendana na mahitaji ya Maisha ya Mwanadamu kulingana na Tabia na Akili zake.
Taikon Acha nipumzike SASA.
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.