Kwa vijana wote ambao upande wao vimekaza

Kwa vijana wote ambao upande wao vimekaza

...idea generally ni nzuri ila,utekelezaji si rahisi kihivyo
..umerahisisha sana!
Sasa mkuu ulitaka niandike kitabu hapa jf? Uzi una limit ya maneno kwaiyo inabidi unaweka abstract ama executive summary basi.
 
Kuna jambo gani la kutafuta fedha lisilo na changamoto?
Hata kula rushwa na kupiga dili pia kuna changamoto mfano angalia vigogo waliopo rumande leo ndio utajua hakuna kitu kisicho na changamoto cha muhimu ni kupambana nazo na si kuzikimbia.
Ha ha ha ha... Duh mkuu punguza ukali wa maneno mdau kashaelewa
 
Hapo umenikuna sana, mimi nipo mjini nimeajiriwa ila napanga mikakati sababu siwezi kujilipua wakati nina familiya inanitegemea. Shamba lazima niende, ndoto zangu zile kubwa zipo huko
 
Sasa mkuu ulitaka niandike kitabu hapa jf? Uzi una limit ya maneno kwaiyo inabidi unaweka abstract ama executive summary basi.
Ukitaka uhondo wa ngoma uingie ucheze, kwani wanaoweza wana nini na wengine washindwe wana nini? Akiamua tu anaweza.
 
Kwanza tutoke mafichoni. Tujitokeze mitaani kuangalia je ni fursa gani zipo. Makala iliyopita nilitoa mfano wa makala ya muuza matunda. Leo naomba nitoe makala nyingine inayofanania.

Kuna rafiki yangu anaishi msata na anajishuhulisha na ufugaji wa ng'ombe wa maziwa. Kuna kijana mmoja alikuwa akisomea masuala ya business administration chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 2013. Yule kijana alikuwa akijaribu kutoka hostel siku za wikiendi na kutembelea maeneo mbalimbali ya mkoa wa pwani.

Katika pitapita yake hakuwahi kuwaambia watu kuwa yeye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam. Katika pitapita hizo akafanikiwa kukutana na yule rafiki yangu anaejishuhulisha na ufugaji wa ng'ombe wa maziwa. Kijana alikuwa muongeaji mzuri na mstaarabu.

Waliongea mengi ila hakumwambia kuwa ni mwanafunzai wa chuo kikuu cha Dar es Salaam anaekaribia kuhitimu.

Alipohitimu alirudi msata kwa yule rafiki yangu. Akamwambia katika pita pita yake ya kutafuta maisha ameona bora aje pale yupo tayari kuajiriwa hata kwa kujitolea ilimradi apate pa kulala pale nyumbani kwa rafiki yangu na huduma za lazima kama chakula, matibabu, etc kama mmoja wa wanafamilia.

Kwakuwa kijana alionekana mstaarabu sana basi alipokelewa. Walifanya wote kazi za pale kwa miezi mitatu na yule rafiki yangu akaona kijana ana upeo mkubwa sana. Akaanza kumdadisi ila kijana hakujielezea elimu yake ya juu alieleza kuwa aliishia darasa la saba.

Huyo rafiki yangu akawa akimtegemea sana yule kijana kusimamia mradi mzima na kijana alikuwa muaminifu sana mpaka ikafika wakati akaanza kulipwa laki3 kwa mwezi.

Yule kijana kwao ni morogoro. Alipopokea kwa miezi sita akaomba akasalimie wazazi. Alipoenda akajenga banda la kutosha ng'ombe kumi wa maziwa kwa kutumia ile 1.8m aloipata.

Akarudi kazini na kuendelea na kazi. Yule rafiki yangu alikuwa pia akiuza ndama mara kwa mara. Kijana alikuwa ndio mtafutaji wateja. Akaanza kununua mmoja mmoja kila mwezi. Ndama mmoja aliuzwa 250,000 na alikuwa akishanunua anatumia 50,000 kumfikisha kwao morogoro.

Baada ya miezi mitano alikuwa na ndama watano kwenye lile banda kule morogoro ambao walikuwa wakihudumiwa na mama yake mzazi kwa pumba na mabua ya mahindi na majani. Mama alipokuwa na pesa kidogo alinunua viambata muhimu madukani kwa ajili ya chakula cha ndama.

Kijana aliukuza mradi wa rafiki yangu ukawa mkubwa kwa miaka mitatu huku nae akiwa na jumla ya ng'ombe 10 kule morogoro wakihudumiwa na mama yake.

Kijana saivi, miaka mitano baada ya kuhitimu, anaendesha miradi miwili, ule wa morogoro na ule wa msata. Wa morogoro ana ng'ombe 15 kwa sasa na kwa wastani anapata lita 200 za maziwa kila siku kule morogoro. Nusu ya mapato yote hurudi kwenye garama za uendeshaji na hubakiwa na pesa ya lita 100 ambayo kwa bei ya 1,000 kwa morogoro hujipatia 100,000 kila siku faida.

Mpango wake ni kuwa na ng'ombe 100 baada ya miaka mitano. Sasa wewe uking'ang'ana na mavyeti na kujibusti utachelewa basi na treni pia litakuacha. Kumbuka safari ya kutembea kwa miguu ni nzito sana usikubali kuachwa na basi na treni pia.

wewe je?
 
Natafuta wataalamu tuwe na kiwanda cha kuhifadhi mbegu za kiume kwny vichupa, wasiotaka kuolewa wajinunulie tu.
Hahahahahaha. Hiyo ndo plani B, yako baada ya maisha kuwa ngumu kumeza. Duuuuuu.
 
Back
Top Bottom