Ali Nassor Px
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,384
- 3,926
Katika maisha ya mwanadamu kuna mambo mengi lakini mawili ni muhimu zaidi.
1. Kujielewa yeye ni nani na anahitaji nini.
2. Kujithamini kabla ya kuthaminiwa.
Ukishafahamu hayo kila kitu utakiweka panapostahiki.
Kuna watu wa kila aina ndani ya jamii zetu.
• Kuna waungwana
• kuna watwana
• kuna wanaohitaji kuelekezwa wakaelewa
• kuna wanaojifanya wajuaji
• kuna wajinga
• kuna wanaowafanya wenzao wajinga
•kuna wenye elimu lakini hawajaelimika
• na kuna wasiojielewa na wala kueleweka.
Wote ni muhimu kuishi nao kwasababu .ili uweze kufahamu hayo inahitaji kitu kimoja tu. Nayo ni kumsafia mtu nia na kumpa nafasi ndani ya maisha yako bila ya yeye mwenyewe kujijua !!!
Kwa sababu mtu mwenye akili ni yule anaeipima nafsi yake na akili yake imefanya nini ?
imekosea wapi ? na imetoa mchango gani mwems katika kustawisha maisha ya wengine anaoamiliana nao.
Binadamu hatakiwi kuwa kama yai bovu,anatakiwa anufaishe na anufaishwe na uwepo wake pahala anapokuwa.
Tunatakiwa kufahamu kuwa tukitathimini thamani ya utu tuelewe kuwa Ihsani hulipwa.Na tusitumie Upole wa mtu vibaya kwani huenda baadhi ya tunavyovihitaji vimo ndani mwa tunao wadharau na kuwaona wa ziada.
Tujitahidi kuyajua ya lazima kwetu na yaliyo na umuhimu ndani ya maisha yetu.✍️