Kwa vile Corona haina kinga wala tiba, Mnaonaje mahospitali yetu pia yakaruhusiwa tutumie tiba asili na tiba mbadala ikiwemo Faith Healing?

Kwa vile Corona haina kinga wala tiba, Mnaonaje mahospitali yetu pia yakaruhusiwa tutumie tiba asili na tiba mbadala ikiwemo Faith Healing?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Janga la Corona ni vita ambayo no one knows its dimensions, hivyo Watanzania hatuna budi kutumia kila silaha, kila mbinu, kila technics, hivyo, baada ya kuisikia ile hotuba ya jana kutokea Ukulu ya Chato, mimi kwa upande wangu naiunga mkono hotuba ile ya Ikulu ys Chato kwa asilimia 100% chini ya 100%, na hili hapa ni bandiko la kuomba maoni yako.

Kufuatia virusi vya Covid-19 vinavyosabisha ugonjwa wa Corona ambao mpaka sasa bado hauna kinga wala tiba, jee mnaonaje kama na mahospitali yetu pia yaruhusiwe tuanze kutumia Tiba Asili na Tiba Mbadala as an alternative medicine, ikiwemo Faith Healing ambapo nchi inayoongoza kwa tiba hizi ni China, na India, wao wanatumia TCM, (Traditional Chinese Medicine), India wanatumia Yoga na meditation, sambamba na Western medicine, kwa huduma ya kwanza ifanyikie majumbani as homeopathy pale tiba asili inaposhindwa the critical ndio wapelekwe mahospitalini, na hii itamaanisha hao ambao tiba asili na tiba mbadala itawagomea, wana issues na kinga zao za miili, ndio wapelekwe hospitali kusubiria hatma zao.

Kwa vile kabla ya ujio wa wakoloni, jamii asili za Tanzania tulikuwa tunategemea tiba asili na tiba mbadala ambapo baadhi ya tiba hizi ni more effective kuliko tiba za kisasa za Wazungu.

Kila kabila lina wataalamu wake wa miti shamba, na kwa wagonjwa ambao wako willing kujaribu tiba asili na tiba mbadala, waruhusiwe kuwa discharged from hospital, warejee nyumbani kujaribu, wakizidiwa warejee hospital, hii itasaidia sana hospitali zetu zisielemewe.

Waganga na mabingwa wa miti shamba wa kila eneo, waliosajiliwa au wanaotambulika na kukubalika na wana jamii husika, waruhusiwe kuingia mahospitalini kuwatibia wagonjwa ambao wako willing.

Zile dawa zitakazo onyesha kuwa very effective, kwa wagonjwa kupata nafuu, wagonjwa waliopona wafanyiwe confirmation test kuthibitisha wamepona kwa dawa ya mganga fulani, kisha mahospitali yafanye sharing of information ya effectiveness, zile dawa zitakazo onyesha kuwa very effective, zifanyiwe clinical test kwa kuwatumia wale wagonjwa critical as Guinea Pigs, kama zitasaidia kutibu.

Zikitibu na kuthibitishwa hao waganga wa tiba hizo wasaidiwe kuwafanyia patent registration tuingie kwenye mass production tuwaokoe Watanzania.

Pia matabibu wote wa faith healing na wachungaji na wahubiri wafanya miujiza ya uponyaji, waruhusiwe kuingia mahospitalini kuwaombea wagonjwa watakaokuwa willing na kuwaponya kwa Jina la Yesu, na watakao pona, confirmation test zifanywe, wakikutwa wamepona waruhusiwe.

Mnaonaje hoja hii?.

Paskali
 
Mkuu, Pascal huja yako ya msingi sana lakini Jana nilishindwa kutoa maoni yangu maana yulitofauti kidogo. Tunahitaji kuchukua hatua kama familia sasa maana Hali sio nzuri niliwahi kutoa uzi hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😱😱😱😱 bila kujua kwanza "COVID-19 genome sequencing" tunapoteza muda tu.
Mungu huwa hakupi kitu unachotaka upewe ila kinachokufaa
 
Dawa kashatoa Rais jana lile futa linapasuka kwa kunawa maji na kujifukiza

P jana ulimzungumzia mwenye PhD (mkemia) aliyewashinda wanasayansi
 
Kutoka uzi mwingine...

Ngoja nkupe elimu nyepesi juu ya cancer, Kuna kitu kinaitwa DNA hii ndo ina determine Kila sehemu ya mwili wako iweje kuanzia yai linapoungana na sperm. Sasa Basi hii DNA iko composed na bases tofauti tofauti mfano guanine, cytocyl, agnine, uracil etc sasa Basi Kuna kitu kinafanyika kinaitwa base pairing rule Ambapo Kila base ina pair na nyenzake in triplets katika kutengeneza tabia za cell za sehemu Fulani mfano kwenye ubongo wa mbele region flani itakiwa uracil, guanine, na cytocyl zi pair na agnine, uracil na thymine ikitokea kwa sababu yeyote Ile maybe yakatokea makosa ikawa tofauti ndo hapo Kuna uwezekano mkubwa ukazaliwa na kasoro au ukajapata cancer ukubwani. Hii ndo sababu kubwa inayoleta cancer. Mimi haya nimeyajua miaka 12 ilopita nikiwa form 6. Sasa wewe unashindwaje hata ku Google ndugu unalishwa matango pori YouTube kirahisi hvo?

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni vizuri kuonesha kisomo, lakini si umepata kusikia 'elimu ni bahari'?

Mapelekeo yake ni kuwa elimu yako inaweza kuwa kisiwa--kisiwa kidogo ama kipana; japo nayo inaweza kana vile kusema: kiko 'kusini' na siyo 'kaskazini' mwa bahari...

Endelea kudadisi na kuchunguza kuzidia misigano ya mawazo na tafsiri za visomo. Wewe una yako na mwenzako anayake -- ukiona 'kuitana majina' hakufurahishi na wala hakupendezei basi jaribu kuheshimiana...

Kuna mazuri kutoka kwa mwenzako aliyeleta habari za chanjo -- chanjo kuwa na 'virusi' vinavyoweza 'kufyatua' maradhi ya saratasi; na kwa kweli ana neno. Hata mimi binafsi nimetia akilini kitu. Bila shaka, kuna wakati nitaunganisha hilo na udadisi kungine...

Sasa, ujue, si lazima mtu awe 'daktari' ili aweze 'kupatia' tiba ya maradhi -- si lazima mtu ajue 'baiolojia' aweze kubaini ni namna gani 'tiba' aambiwayo inafanyakazi. Hili linataka 'busara' zaidi na si 'maarifa'.

Watu humu Jamiiforums kwa mfano, wanakebehi mno Rais Magufuli anavyopendekeza 'tiba ya kujifukiza'... Wengi ya hawa, pasi shaka, 'wanajiona wana maarifa' lakini kwa kweli wamekosa busara. Tena, humu nimeona hata baadhi ya vipande vya habari vinavyoonesha kuna 'wataalam wa afya' pia wamepata kubeza namna hii ya tiba kwa majibu ya haraka haraka kwamba eti, na kwa kupangilia upya maneno, kana kudai: 'pua haijaumbwa kuingiza namna ya kitu cha moto'... Hii ni kasumba! Hii ni kwa sababu wataalam wetu hawa wa 'kuigizia igizia' -- tabia ya 'muuonekano wa kitaalam' ama mara nyingine muonekano wa 'kiuongozi ongozi' -- wamekosa nidhamu na haiba ya kujifunza hata yaliyo nje wa wigo wao wa mazoea na maisha yote kwa ujumla.

'Elimu nzima' kwa mwadamu inahitaji haiba zote mbili -- 'werevu' na pia 'upole'... 'Ukijifanya wewe mwerevu sana -- kupiliza' nasi ujue : "kuna njia ionekanayo kana ni sahihi sana katika jicho la mwadamu na hali hiyo ni ya kuelekea mauti'... Kuwa 'mtoaji' kadri ifaavyo sana wewe pia kuwa ni 'mpokeaji'.

Sasa, kwa mfano, hao waliotajwa na Rais kupulizia 'kitakasa hewa' wanatumia busara ipi kujibu ama kujitetea ikiwa hawana haiba ya 'kujishusha' ili maarifa yao na busara yao ifanye utetezi wa haki? Je, ni chumvi kloreti maji ilitumika ama klorini maji? Walifanya jukwaa sahihi la wataalam na washikadau/wananchi kukidhi taratibu bora na mipango, ushirikishwaji na uendelevu panapo uwazi pia?

Rais hakuhitaji hata kudokeza uhusiano wa 'virusi' na 'mvuke' kimawezekano ya kikemia -- kusema kana vile labda mvuke unaweza kusambaratisha mjengeko wa virusi... Mchanganyiko wa namna ya mizizi na viungo kama vile tuseme tangawizi, vitunguu saumu, maganda ya ndimu ama limau, katika mchemsho, na kujifukiza ni namna ya 'sanaa ya tiba' ambayo katika utamaduni na ustaarabu wa kileo tunaita tiba hii kuwa ni 'mbadala'... Sasa, ulimwengu wa tiba, hii mbadala, una sifa na kanuni zake ambazo SI LAZIMA ushahibiane ama kufanana na kanuni na utaratibu wa tiba za 'kisomi' -- japo nayo ina kisomo chake -- kinachotaka hasa mtu awe na hiyo sifa ya 'werevu' na 'upole' ili kujifunza na kukomaa katika sanaa ya tiba husika.

Sasa, Saratani ugonjwa ambao unaweza kutibiwa kwa namna ya sanaa za tiba. Hakuna ugonjwa usiyo na dawa katika ulimwengu huu labda iliwa kwa ujinga, uzembe, kutowajibika -- hatujali kujiongeza ili kujitibu kwa maradhi yanayotusibu. Daima ikiwa tiba hakuna katika 'utaalam' tiba za visomo madarasani basi ipo kwenye upande wa tiba mbadala... Mjinga yeyote na Mwenyekasumba aendelee kujikwamisha kwa msala wake wa kutopanua wigo wake wa maarifa na busara...

Nilipata kuwahudumia wateja fulani ofisini kwangu mapema wiki hii... Hawa walikuwa ni waganga wa tiba za jadi waliokuwa wakichakata barua zao za kuomba kibali wizarani kuzijaribisha dawa zao ili zitimike kwa kutibu maradhi ya virusi vya covid19; nilijikuta nikiingilia kati mazunguzo yao kwa nasaha mbili tatu. Kati ya wawili hawa, mmoja alikuwa kana analalamika, akiwa kama, kiongozi mwakilishi -- maombi ni mengi halafu watu wake wanadhani kama ni jambo rahisi wao kupewa nafasi hiyo... Ilibidi nizungumze na huyu ndugu na kumueleza: ni haki ya kila mtu mwenye kudhani anayo 'dawa' kwa tatizo hili kupewa nafasi; tatizo ni labda 'ukomo wa rasilimali' zilizopo ama ukiritimba wa kitaasisi. Na kwa kuwa nilihisi kulikiwa na kubezana, nilimwambia tiba za jadi / mbadala si za namna ya tiba za kisomi kusema wanahitaji 'maabara' ama kujua eti 'kirusi cha covid19' kinafananiaje...Maabara ya mtaalam wa tiba za jadi ni kichwa chake, utaalam/uzoefu -- na kile hata pale walikuwa wakikitaja kama 'mizimu'... Sasa binafsi ninajua mengine ambayo pale hapakuwa muafaka 'kubadilishana maarifa' na 'visomo mbadala'... Lakini nilipata kuaminiwa na wao kunieleza jinsi wanavyohisi kuna 'njama za madaktari(waandamizi kiwadhfa labda?)'-- daima huwa wanadumisha ama kukuza majanga ili wapate 'chochote'... Najua hili si kwa madaktari tu bali watu wa kada zote na kwa nafasi zao -- tuna shida hii -- binadamu kwa nafsi zetu za chini tuna nasibu ya 'makusudio yenye kuharibika'... Na, nikapewa mfano; mmoja wa hawa wawili amewahi kuwa karibu na waziri ambaye kwa nafasi yake alikuwa anasumbuliwa takwimu zinazoendelea kuwa mbovu za 'mlipuko wa ugonjwa wa kuhara'... Yeye akamshauri, mheshimiwa, wewe tangaza tu sasa kuwa janga limekwisha halafu uone... Akacheka na kusema, ni kweli alipotangaza na takwimu mbovu mbovu zikapungua na kuisha!

Uongozi ni zaidi ya maarifa -- busara inahitajika na wakati mwingine kiongozi hafananii kukubaliana na 'wataalam' katika maamuzi. Japo wote, tukiwa na busara, tunatambua kila mtu atawajibika na maamuzi yake kwa jema ama baya... Labda ni wajibu wa mwenyebusara yoyote kutetea uamuzi ama shauri la mwingine linaloonekana kufanyika katika 'busara' fulani...

Na basi kwa namna hii hii, mimi kama mtu, pia ni mtetezi wa matumizi ya 'mafuta ya bangi' katika tiba ya saratani...

Sasa, werevu waliokosa busara wasijidai 'kujua' sana-- oh, lakini tuna Hospitali ya kisasa ya 'Ocean Road' -- mapesa mengi kweli yamewekezwa pale na mafunzo ya hali ya juu ya sayansi ya tiba ya mionzi inaendelea...

Kupanga ni Kuchagua; ukipanga na utaalam wa upande mmoja itakusaidia nini hata kama 'Wafadhili' watakupatia msaada wa 'matrillioni ya dola'(?). Yale yale... 'Pasu kwa pasu' itahusika -- pesa nyingi itaiishia 'mifukoni' mwa watu... Tiba itangojea...
 
Tiba ya asili ipo kwa waganga wa kienyeji, faith healing ipo kwa manabii na mitume wa siku hizi, hospitalini wacha zibaki tiba za kizungu.

Utabeba vipi mitishamba upeleke hospitalini, au na wewe uko spidi kama mwenzako wa ile kanda yenu?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moja ya kitu kibaya walichotufanyia wakoloni ni kutuaminisha dawa zetu ni za kishenzi kupitia dini zao lakini kwa wenzetu wa asia pamoja na kupokea dini zao hawakuacha tiba zao za asili ndio maana tunahangaika na tiba za kichina wakati tulikuwa na tiba zetu
 
Muhimbili kuna kitengo cha tiba za asili lakini serikali haipeleki pesa kwa ajili ya utafiti wa madawakuna magonjwa kama kansa, sukari, figo yanatibiwa kwa tiba asili wakati hospital yameshindikana
 
Wanabodi,
Janga la Corona ni vita ambayo no one knows its dimensions, hivyo Watanzania hatuna budi kutumia kila silaha, kila mbinu, kila technics, hivyo, baada ya kuisikia ile hotuba ya jana kutokea Ukulu ya Chato, mimi kwa upande wangu naiunga mkono hotuba ile ya Ikulu ys Chato kwa asilimia 100% chini ya 100%, na hili hapa ni bandiko la kuomba maoni yako.

Kufuatia virusi vya Covid-19 vinavyosabisha ugonjwa wa Corona ambao mpaka sasa bado hauna kinga wala tiba, jee mnaonaje kama na mahospitali yetu pia yaruhusiwe tuanze kutumia Tiba Asili na Tiba Mbadala as an alternative medicine, ikiwemo Faith Healing ambapo nchi inayoongoza kwa tiba hizi ni China, na India, wao wanatumia TCM, (Traditional Chinese Medicine), India wanatumia Yoga na meditation, sambamba na Western medicine, kwa huduma ya kwanza ifanyikie majumbani as homeopathy pale tiba asili inaposhindwa the critical ndio wapelekwe mahospitalini, na hii itamaanisha hao ambao tiba asili na tiba mbadala itawagomea, wana issues na kinga zao za miili, ndio wapelekwe hospitali kusubiria hatma zao.

Kwa vile kabla ya ujio wa wakoloni, jamii asili za Tanzania tulikuwa tunategemea tiba asili na tiba mbadala ambapo baadhi ya tiba hizi ni more effective kuliko tiba za kisasa za Wazungu.

Kila kabila lina wataalamu wake wa miti shamba, na kwa wagonjwa ambao wako willing kujaribu tiba asili na tiba mbadala, waruhusiwe kuwa discharged from hospital, warejee nyumbani kujaribu, wakizidiwa warejee hospital, hii itasaidia sana hospitali zetu zisielemewe.

Waganga na mabingwa wa miti shamba wa kila eneo, waliosajiliwa au wanaotambulika na kukubalika na wana jamii husika, waruhusiwe kuingia mahospitalini kuwatibia wagonjwa ambao wako willing.

Zile dawa zitakazo onyesha kuwa very effective, kwa wagonjwa kupata nafuu, wagonjwa waliopona wafanyiwe confirmation test kuthibitisha wamepona kwa dawa ya mganga fulani, kisha mahospitali yafanye sharing of information ya effectiveness, zile dawa zitakazo onyesha kuwa very effective, zifanyiwe clinical test kwa kuwatumia wale wagonjwa critical as Guinea Pigs, kama zitasaidia kutibu.

Zikitibu na kuthibitishwa hao waganga wa tiba hizo wasaidiwe kuwafanyia patent registration tuingie kwenye mass production tuwaokoe Watanzania.

Pia matabibu wote wa faith healing na wachungaji na wahubiri wafanya miujiza ya uponyaji, waruhusiwe kuingia mahospitalini kuwaombea wagonjwa watakaokuwa willing na kuwaponya kwa Jina la Yesu, na watakao pona, confirmation test zifanywe, wakikutwa wamepona waruhusiwe.

Mnaonaje hoja hii?.

Paskali
Wandugu, hapa nafanya tuu follow up ya Corona nikipitia kujikumbusha niliwahi kuandika nini au kusema nini kuhusu Corona na hiki kinacho endelea sasa. Corona is real tusifanye masihara, tujilinde kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Kila Jumamosi asubuhi kuanzia saa 1:30 hadi saa 3:00 asubuhi , Star TV, huwa ninakuwa live kwenye kipindi cha TV cha Jicho Letu Ndani ya Habari ambacho huwa kinatangwa live na Star TV kila siku za Jumamosi asubuhi, kwa Jumamosi ya kesho, mgeni wetu ni Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe tukijadili kuhusu athari za Corona kwenye sekta ya Habari, nini kifanyike.

Ukipata nafasi karibu utufuatilie.

P
 
Back
Top Bottom